JAMHURI YA KENYA WIZARA YA KILIMO, MIFUGO, UVUVI NA UNYUNYIZAJI (MoALFI) IDARA YA SERIKALI YA UVUVI, KILIMO CHA MAJINI NA UCHUMI WA RASILMALI ZA MAJINI (SDFA-BE) MCHAKATO WA MWISHO MAENDELEO MRADI WA MAENDELEO YA KIJAMII NA KIUCHUMI WA UVUVI WA BAHARINI KENYA (KEMFSED) TAREHE 18 - 19 JUNI, 2019 MCHAKATO WA MAENDELEO MRADI WA MAENDELEO YA KIJAMII NA KIUCHUMI WA UVUVI WA BAHARINI KENYA (KEMFSED) Imeandaliwa na KWA USIHIRIKIANO NA << MCHAKATO WA MAENDELEO >> Usuli 1. Mradi wa Maendeleo wa Kijamii na Kiuchumi wa Uvuvi wa Baharini Kenya (KEMFSED) unalenga kufanikisha manufaa ya kiuchumi kutoka kwa rasilimali za pwani na za baharini. Lengo la Mradi huu wa Maendeleo ni kuimarisha usimamizi na kuzidisha uongezaji wa thamani wa kipaumbele cha uvuvi na kilimo cha baharini, kuboresha ufikiaji wa riziki za jamii za pwani ya Kenya. Mradi huu utatekelezwa na Serekali ya Kenya (GoK) kupitia Idara ya Uvuvi, Kilimo cha Majini na Uchumi wa Rasilmali za Majini (SDFA&BE) kwa usaidizi wa Benki ya Dunia. Eneo la pwani na baharini ambalo uchumi wa rasilmali za majini ulijengewa lina matumizi mengi tofauti, baadhi yake kwa sasa yakiwa haribifu na yenye kukosa uendelevu, na mengine yanaweza kuzalishwa upya, baadhi yake pia ni ya kipekee na mengine yanaingiliana . Upeo wa Kijiografia wa Mradi Huu 2. Mradi wa KEMFSED utahusisha kaunti tano (5) za pwani ambazo hugusa mwambao wa Bahari ya Hindi. Kaunti hizi zimechaguliwa ili kunufaika kutokana na mradi; nazo ni Kwale, Mombasa, Kilifi, Tana River na Lamu. Vipengele vya mradi 3. Vipengele vya mradi vimebuniwa ili kufaa kwa upana katika muundo wa Uchumi wa Rasilimali za Majiini na katika mchakato unaoendelea wa ugatuzi. Vipengele vikuu na vile vidogo viliboreshwa na kupangwa upya ile kuimarisha mwelekeo, mtiririko, ujumuishaji na usawishaji bora wa vipengele vigumu/muundo msingi kwa msaada mwepesi/ wa kiufundi, mafunzo na kuwajenga watu uwezo. Mchoro wa 1: Nadharia ya Mabadiliko ya Mradi wa KEMFSED Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 3 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> Kipengele cha 1 - Kuimarisha Uongozi na Usimamizi wa Uvuvi wa Baharani. 4. Hili linalenga kuimarisha usimamizi wa uvuvi wa baharini kwenye bahari ya Kenya. a) Kipengele kidogo 1.1 Kuboresha uongozi wa uvuvi wa baharini na uchumi wa rasilimali za majini. Kipengele hiki kidogo kitalenga kuimarisha uongozi na usimamizi wa uvuvi, ukaguzi wa sera ya uvuvi na sheria husika, na kuimrisha ufuatiliaji na uangalizi. Kipengele hiki kidogo pia kitalenga utafiti unaohitajika ili kuimarisha usimamizi wa uvuvi wa baharini, pamoja na kuunda Mfumo bora wa Taarifa za Uvuvi na Ufuatiliaji (FIMS) ambao utawezesha upatikanaji wa habari kwa minajili ya kuwa na usimamizi bora wa uvuvi. Vinapotambuliwa, vipaumbele vya uvuvi vitalengwa kwa minajili ya kuchukua hatua zinazoendana na Mipango ya Kuimarisha Uvuvi (FIPs), kwa lengo la kufanya uvuvi huu kuwa na usimamizi bora, hivyo kuhakikisha manufaa endelevu ya muda mrefu kwa jamii husika. Mradi huu pia utasaidia ukuzaji wa Mipango ya Kitaifa ya hatua dhidi ya papa, ndege na uvuvi Haramu, Uvuvi Usioripotiwa na Usiodhibitiwa (IUU). b) Kipengele kidogo 1.2 Kuboresha usimamizi wa uvuvi wa karibu na ufukoni. Kipengele hiki kidogo kitaimarisha usimamizi wa uvuvi wa karibu na ufukoni na hata utekelezaji wa Mipango ya Usimamizi wa Uvuvi (FMPs). Kwa kufanya kazi pamoja na FMPs za kitaifa za uvuvi wa kipaumbele, kiungo kipya cha Msimamizi wa pamoja wa Maeneo (JCMAs) utaanzishwa, na usimamizi uliokuwepo kuimarishwa. Mradi huu pia utasaidia utekelezaji wa Eneo Linalosimamiwa kwa Pamoja (CMA) ukiwemo utekelezaji wa mikakati ya Ufuatiliaji, mikakati ya Udhibiti na Uangalizi (MCS) na utoaji wa vifaa vinavyohitajika na msaada wa kiufundi kwa MCS. Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 4 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> c) Kipengele kidogo 1.3 Kujenga muundo msingi wa usimamizi wa uvuvi. Kipengele hiki kidogo kinajumuisha ustawishaji wa muundo msingi ambao unalenga hasa kusaidia katika usimamizi wa uvuvi katika ngazi ya kitaifa na kaunti. Mahususi, kinajumuisha jengo litakalokuwa na ofisi ya Huduma ya Uvuvi Kenya (KeFS) Nairobi, na Kituo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Rasilimali za Baharini katika Kaunti ya Kwale. Mfano wa muundo msingi wa uvuvi unaweza kujumuisha kuboresha ofisi za uvuvi za kaunti, na kupanua Chuo cha Mombasa Bandari Maritime Training College. Kipengele 2 - Kuwezesha Uwekezaji Endelevu katika Uvuvi wa Baharini na Kilimo cha Majini. 5. Hili litaanzisha Huduma ya Kustawisha Biashara Ndogo ndogo na za Wastani (SME-DS) ambazo zinatoa ufikiaji wa utaalamu kwa wajasiriamali, SMEs na mamlaka katika kaunti za pwani, na hata kuwezesha kuzidisha thamani inayotokana na uvuvi na kilimo cha baharini kwa kuwekeza katika muundomsingi ya umma kama vile barabara, umeme, usambazaji wa maji, unaohusiana na minyororo mahususi ya thamani na uwekezaji wa kibinafsi. a) Kipengele kidogo 2.1: SME-DS katika Jamii za Pwani. SME-DS itakodishwa ambayo imeundwa na kikundi cha wataalam wa maendeleo yanayohusiana na SME na ambayo inapatikana kwa jamii za wavuvi katika pwani ya Kenya. Wataalamu hawa wataimarisha huduma zao katika Vitengo vya Usimamizi wa Ufukoni (BMUs) na kwa wakaazi wa pwani ambao wangependa kuanzisha au kupanua biashara zinazohusiana na uvuvi na pia kutoa usaidizi wa kiufundi kulingana na mahitaji, huduma za uchambuzi, kujengea watu uwezo na huduma za kushiriki maarifa. SME-DS pia itatambua hatari za kimfumo au masuala ambayo huzuia miradi iliyo na uwezekano wa kunawiri kuwa tayari na itapendekeza suluhu zinazohitajika kuondoa au kupunguza hatari kama hizo. Mafunzo na mwongozo kuhusu ufikiaji wa vyanzo vilivyopo na vinavyoibuka vya mikopo pia itajumuishwa. Kipengele hiki kidogo pia kitasaidia SMEs ambazo zingependa kuanzisha huduma ili kuongeza thamani na kuwa na minyororo ya thamani ya uwazi ya vyakula vitokavyo baharini. Aidha, mradi huu utatoa msaada wa kiufundi ili kuongoza uanzishwaji na utendaji kazi wa Mamlaka ya Soko la Samaki Kenya. b) Kipengele kidogo 2.2: Kuimarisha muundo msingi wa uvuvi na kilimo cha baharini ili kukuza Minyororo ya Thamani. Kipengele hiki kidogo kitalenga mianya iliyotambuliwa kwenye kaunti katika muundo msingi wa kimsingi wa umma (maji, umeme, uchukuzi) ambayo inazuia nafasi za uwekezaji wa kibinafsi katika uvuvi wa baharini na kilimo cha baharini. Ili kuhakikisha kuwa uwekezaji wote umehalalishwa kwa uwazi, na kusaidia uwekezaji wa kibinafsi wa ziada, na kupunguza uwezekano wa kuchochea juhudi za uvuvi wa kupita kiasi, minyororo yote ya thamani inayohusiana na muundo msingi wa umma ambayo ilipendekezwa na kaunti kulingana na mpango wa kuanzisha muundo msingi wa uvuvi na kilimo cha baharini wa kaunti. Hatari zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi zitajumuiswa katika uundaji wa uwekezaji wote wa muundo msingi. Kipengele 3 - Kuwezesha Jamii za Pwani na Riziki. Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 5 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> 6. Kipengele hiki kitalenga kuimarisha riziki ya jamaa maskini katika jamii za pwani, na kuwezesha wavuvi kuzingatia hatua za usimamizi wa uvuvi. Mbinu ya kijumla ambayo inalenga kukuza riziki za ziada, itafuatiliwa, kwa kuanzisha ushirikiano muhimu na biashara mpya au zilizokuwepo na kwa kuzingatia mkataba wa mipango ya kilimo na kilimo cha majini ambayo inanufaisha wazalishaji wadogo. Kwa upana zaidi, miradi midogo ya kutoa riziki ndogo ndogo ambayo imetekelezwa na watu binafsi au na vikundi vidogo vya wafanya biashara, itasaidiwa kupitia kwa utoaji wa ruzuku, msaada wa kiufundi, na mafunzo ya kibiashaa na ya ujuzi. a) Kipengele Kidogo 3.1: Kuboresha Riziki ya Jamii za Pwani. Kipengele hiki kidogo kinajumuisha fedha ya ruzuku inayotoa msaada wa kifedha kwa wafadhiliwa wanaofaa kupitia njia tatu za kipekee: i)ruzuku za miradi midogo ya wazalishaji wanaofaa wa mapato madogo wa pwani; ii) Ruzuku ya miradi midogo ya jamii ya kijamii na kimazingira (mtaji asili) na iii) ruzuku za kuongeza mtaji kwa vikundi vya vijijini vinavyoweka akiba na kutoa mikopo (VSL). b) Kipengele Kidogo 3.2: Kusaidia Huduma za Kuboresha Riziki na Kujengea Watu Uwezo. Itatekelezwa na kaunti husika, kipengele hiki kidogo kitatoa huduma za kusaidia na kujenga uwezo kwa vikundi vinavyofadhiliwa ambavyo vinahitajika kutekeleza, kukamilisha shughuli ambazo zimetekelezwa chini ya kipengele kidogo 3.1 ikijumuisha: i) huduma na msaada wa kiufundi (TA) iliyotolewa ili kutambua wapokeaji wa ruzuku na matayarisho yanayosaidia, usimammizi na uangalizi wa miradi midogo; ii) kutoa mafunzo ya ujuzi na biashara kwa wapokeaji wa ruzuku na biashara zingine ndogo; iii) Programu ya akiba ya vijijini na mikopo (VSL); na iv)Udhamini wa ujuzi rasmi, mafunzo ya ufundi na elimu ya kitaaluma. Kipengele 4 - Usimamizi wa Mradi 7. Kipengele hiki cha 4 kitagharamikia msaada ya ziada wa usimamizi wa mradi katika ngazi ya kitaifa na ya kaunti ili kuhakikisha kuwa shughuli za kutekeleza mradi zinafanywa kwa utaratibu na kwa wakati. Mahususi, kitasaidia katika uangalizi wa mradi na uratibu kwa ikiwemo kufanikisha shughuli za Kamati inayoendesha ya Mradi wa Kitaifa (NPSC) na Kamati ya Mradi ya Ushauri wa Kiufundi (PTAC); kuanzishwa na kuendeshwa kwa Vitengo Vya Uratibu wa Mradi (PIUs) katika ngazi ya kaunti, ikijumuisha utoaji wa vifaa; usimamizi wa kimaadili, udhibiti wa ubora na mifumo ya bima; usimamizi wa utunzaji wa kimazingira na kijamii; na ukaguzi wa kiufundi kama inavyohitajika. Kipengele hiki pia kitagharamikia matayarisho na utekelezaji wa mkakati wa mawasiliano, na utekelezaji wa mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini. (M&E), ambao utahitaji kutekelezwa ili kupata data kuhusu ufanisi wa vitu mahususi na wa kifedha, utendaji kazi wa shirika tekelezi na taasisi zingine/watoaji huduma, na matokeo yaliyopatikana kuhusiana na mapato na matokeo. Aidha, itasadia katika kuunda Utaratibu wa Kushughulikia Malalamiko na kuhakikisha kuhusishwa kwa raia. Wanaonufaika na Mradi Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 6 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> 8. Mradi huu utatoa jibu kamilifu kwa matatizo mengi ambayo hukabili jamii za pwani wavuvi walio maskini na wenye uwezo wa kuathirika kwa urahisi. Vikundi wenye kufaidika kutokana na mradi ni wavuvi na familia maskini zaidi zinazotegemea wavuvi katika katika kaunti 5 ya pwani. Ushirikishwaji wa kijamii kama kanuni ya utekelezaji wa mradi huu utajumuisha watu wenye uwezo wa kuathirika kwa urahisi na vikundi vilivyotengwa, na uanishaji wa makundi haya utabainishwa na kikundi kinachosimamia mradi. Hawa ni pamoja na wakongwe maskini, walemavu, jamaa zinazoongozwa na watoto, watu walio na maradhi ya UKIMWI, watu wanaopata nafuu kutokana na uraibu wa dawa za kulevya, vijana, wanawake, wajane, wanaume waliofiwa, jamii zilizo na watu wachache miongoni mwa mengine. Malengo ya Mchakato wa Maendeleo 9. Mchakato wa Maendeleo utatumika kama mwongozo ambao utaimarisha shughuli na harakati zinazohusiana na KEMFSED ili kujumuisha maslahi na mahitaji ya jamii za pwani na wahusika wakuu. Unashughulikia ushiriki muhimu wa watu ambao wanaweza kuathiriwa wakati uamuzi utafanywa kudhibiti ufikiaji wa maliasili katika maeneo ya pwani ya Kenua yaliyo chini ya mradi huu. Lengo la Mchakato wa Maendeleo ni kuhakikisha kwamba maeneo ya pwani yanasimamiwa vizuri kwa lengo la kuhifadhi maliasili na tamaduni za wakazi na kwa wakati huo huo, kuhakikisha kwamba watu wanaoathirika wanachukua jukumu muhimu katika maamuzi na katika kuamia na kutekeleza vibadala vya kurejesha au kuboresha upataji riziki na mapato yanayoathiriwa na uamuzi husika. Lengo ni kuhakikisha kwamba hakuna yeyote ataachwa katika hali mbaya kwa sababu ya Mradi. 10. Kulingana na mwongozo wa OP/BP 4.10, lengo la mchakato wa maendeleo ni kuanzisha mchakato ambapo watu wa jamii ambazo zinaweza kuathirika na mradi wanahusishwa katika upangaji wa vipengele vya mradi, uamuzi wa hatua zinazofaa kuchukuliwa ili kutimiza lengo la kuwapa makao mbadala, na utekelezaji na ufuatiliaji wa malengo ya mradi. (Soma OP 4.12, aya za 7 na 31). Kimahususi, mchakato wa maendeleo hufafanua hatua za kufanikisha utekelezaji wa mradi. Umuhimu wa Mchakato wa Maendeleo 11. Mchakato huu wa Maendeleo umeandaliwa kwa sababu KEMFSED inaweza kudhibiti ufikiaji wa maliasili katika mbuga na hifadhi zinazolindwa kisheria. 12. Ufadhili wa Benki ya Dunia kwa KEMFSED unahitaji kwamba Mradi ufuate Sera za Ulinzi wa Benki ya Dunia ili kuhakikisha kwamba hakuna madhara yasiyostahili kwa watu na mazingira yao kutokana na Mradi huu. Imetambuliwa kwamba KEMFSED inagusia Sera ya Ulinzi wa Benki ya Dunia inayohusu Kuhamishwa Bila Kukusudia (OP/BP 4.12) kwa sababu ya shughuli zilizo chini ya Kipengele cha 1,2 &3. Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 7 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> 13. Vipengele hivi vitahusisha uungaji mkono wa utekelezaji wa mradi wa KEMFSED ambao hatimaye, utaathiri utumiaji wa maliasili ya pwani, Maeneo ya Bahari Yanayolindwa na unaweza kusababisha “kupotea kwa mali na ufikiaji wa mali” kwa kaya zit akazohusika. Katika hali hii, kuanzisha Sera ya Ulinzi wa Benki ya Dunia inayohusu Kuhamishwa Bila Kukusudia (OP/BP 4.12) kunahitaji kubuni Mchakato wa Maendeleo ambao utakuwa mwongozo wa kusaidia kushiriki kwa watu wanaoathirika katika uandaaji wa shughuli za mradi na kuhakikisha kwamba jamii zinazoathiriwa zina fursa za kuboresha au angalau kurejesha riziki na viwango vyao baada ya kuhamishwa. 14.Kwa sababu ya kuhamishwa bila kukusudia na vikwazo vinavyowekewa ufikiaji wa rasilimali katika mbuga na hifadhi zinazolindwa kisheria matukio ambayo yanaweza kusababisha changamoto kubwa za kijamii na kiuchumi kwa jamii husika, sera ya Benki ya Dunia OP 4.12 inahakikisha utoaji wa ulinzi pale ambapo serikali inadhibiti ufikiaji wa rasilimali katika mbuga na hifadhi zilizo katika maeneo yanayolindwa. ushiriki wa jamii katika utekelezaji wa mradi 15. Lengo la kijumla la KEMFSED ni kuimarisha manufaa ya kiuchumi na riziki za watu wa pwani kutokana kwa uvuvi wa baharini na kilimo cha majini cha pwani, huku ikilinda uadilifu mifumo ya ikolojia. Ili kutimiza lengo hili ni muhimu kuhakikisha kwamba shughuli za mradi zina utimamu wa kimazingira na kijamii na ni endelevu, kwamba haki na maslahi ya Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika yaliyo katika maeneo ya mradi yanalindwa na shughuli za mradi zizingatie sera mbalimbali za Ulinzi wa Benki ya Dunia kama vile OP 4.01, 4.10, 4.12 na Sera nyingine za Utendakazi za Benki ya Dunia zinazoweza kugusiwa na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mradi. Kwa hivyo uungaji makinifu wa jamii ni muhimu katika kupata mpangilio endelevu wa utumiaji wa rasilimali na kupunguza na kudhibiti madhara yanayoweza kutokana na shughuli za mradi. Ili kutimiza hilo, kuhusisha na kufadhili ushiriki wa jamii ni muhimu katika ushiriki wao. Ushiriki na mashauriano kwa jamii zilizo katika maeneo yatakayoathiriwa na mradi wa KEMFSED utaratibiwa kupitia utekelezaji wa mradi. Mtazamo wa Uhusishaji wa Jamii 16. Yafuatayo yanafaa kuzingatiwa wakati wa kuhusisha jamii: a) Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika pamoja na jamii nyingine kubwa wanazoishi nazo yanafaa kuchukuliwa kuwa wanufaika sawa wa mradi na juhudi sharti zifanywe ili kushughulikia hali zinazobagua kati yao na jamii za wengi wakati wa utekelezaji wa mradi wa KEMFSED. Maoni ya jamii zote zinazoathiriwa na mradi yatazingatiwa na kuheshimiwa. b) Wavuvi na jamii za wavuvi zinachukuliwa kuwa washirika na wadau wenye usawa katika utekelezaji wa miradi ya KEMFSED. Maoni yao yatazingatiwa na kuheshimiwa. Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 8 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> c) Ni muhimu kutowapa wanajamii matumaini ambayo mradi hautaweza kutimiza. Mradi utahakikisha kwamba jamii zinaarifiwa kikamilifu kuhusu upeo wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mradi na matokeo yanayotarajiwa. d) Jamii za pwani zina makundi mbalimbali ya watu yanayotofautiana kwa utamaduni na desturi, viwango mbalimbali vya kutegemea maliasili, viwango vya elimu pamoja na kujihusisha katika shughuli tofauti za kuchuma mapato. Pia zina majukumu tofauti kulingana na jinsia mambo ambayo yanaweza kuathiri ushiriki wao katika mradi. e) Ni sharti wanajamii washauriwe kikamilifu wakati wa kuandaa, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za mradi. Ingawa huenda wasiwe na ujuzi wa kiufundi wa kushiriki katika shughuli za mradi, ufahamu wao wa jadi utajumuishwa katika muundo mzima. f) Inatambuliwa kwamba kuhusisha jamii za wenyeji ni mchakato unaochukua muda na unaohitaji subira na kutotetereka. Uwakilishi wa Jamii Zinazoathiriwa 17. Ingawa mashauriano yatafanyika ili kuhakikisha ushiriki wa jamii katika kuandaa usimamizi na kuanzisha mipaka mipya ya shughuli za uvuvi, ni muhimu pia kuhakikishwa kwamba wanajamii wanaendelea kuhusishwa katika ngazi za juu za mradi. Wanajamii wataombwa kuwa wanakamati wa kamati za ushauri katika kila eneo la kutia nanga na bandari. Mahali ambapo kamati hizo tayari zipo, zitatiwa nguvu kwa kuhakikishwa kuwa jamii zinawakilishwa kwa usawa na kwamba kamati hizo zinafanya kazi kulingana na hadidu zao za rejea. Mfumo huu utatoa fursa kwa jamii zinazotegemea bahari na maliasili ya uvuvi kujihusisha kimahususi na wadau wengine ili kuchangia katika mchakato wa upangaji na pia kuwa na nafasi ya kutekeleza shughuli za mradi na uhusika wa muda mrefu katika utumiaji endelevu na uhifadhi wa maliasili ya bahari mbali na kudumisha uimara wa ikolojia ya pwani. Isitoshe, viongozi waliochaguliwa jamii za eneo la mradi wakiwemo wale wa Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika watawakilishwa kwa usawa katika kamati elekezi ya mradi, kamati hiyo itakuwa na jukumu la kufuatilia mradi katika ngazi za kaunti na jamii. Utambuzi na Ustahiki wa Watu Watakaohamishwa 18. Fasili ya Watu Wanaohamishwa ni kwa mujibu wa mwongozo wa Benki ya Dunia OP 4.12, kauli “watu wanaohamishwa” ni kisawe cha “watu wanaoathirika na mradi” na halihusu wanaohamishwa kutoka sehemu moja tu. Ikumbukwe kwamba shughuli za mradi hakitasababisha watu au jamii kuondolewa moja kwa moja mahali walipo. Kwa hivyo watu wanaohamishwa ni wale wanaoathiriwa na mradi kwa namna iliyoelezwa katika aya ya 3b ya OP 4.12. Neno hili linawagusia watu wote ambao watapoteza “uwezo wa kufikia maeneo ya mbuga na hifadhi yanayolindwa kisheria na hivyo kuathiri vibaya njia zao za kupata riziki.” Ni muhimu kukumbuka kwamba si kila mvuvi atastahili kupata usaidizi wa riziki chini ya mradi, kwa sababu dai la kupoteza ufikiaji kwa sababu vya udhibiti unaofanywa chini ya mradi sharti lithibitishwe. Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 9 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> Kubainisha Athari kwa Wanajamii 19. Ingawa inatarajiwa kwamba mradi utaathiri riziki ya wanajamii kwa kuweka vikwazo katika rasilimali,kwa mfano udhibiti wa uvuvi haramu, uvuvi wa kupindukia au uvuvi usiodhibitiwa pamoja na kuhamishwa wakati wa upanuzi wa maeneo ya kutia nanga au bandari za wavuvi, kuanzishwa kwa sheria na kanuni mpya katika usimamizi wa fuo au kutekelezwa kwa sheria na kanuni zilizopo, athari kwa wanajamii mahususi kama vile wanawake, Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika, miongoni mwa wengine hakutafahamika kikamilifu hadi wakati shughuli za mradi zianze. Ili kubaini athari hizo kikamilifu, itakuwa muhimu kushirikiana na wanajamii, wavuvi na mashirika yanayowawakilisha katika kutambua wanaoathirika moja kwa moja na kufahamu njia ambazo athari hizo zinawafikia na mbinu za kuzidhibiti. Hili litafanyika kwa kuzihusisha jamii kwa njia mbalimbali. Kwa mfano, kufanya ufuo wa Shimoni uwe wa kisasa unaweza kusababisha vikwazo vya usafiri kutoka visiwa vya Wasini na Mukwiro kuelekea Kwale, wenye mitumbwi wanaweza kupoteza riziki kwa sababu ya kupanuliwa kwa bandari ya uvuvi na kuwepo kwa sheria na kanuni mpya pamoja na kuletwa kwa boti mpya za kisasa kwa ajili ya utalii na usafiri wa wenyeji. Isitoshe, upanuzi na kufanya fuo za uvuvi ziwe za kisasa kunatarajiwa kutasababisha kuanzishwa kwa sheria mpya za usafi na labda ada ambazo zinaweza kufanya iwe vigumu kwa kina mama karanga kuendelea kuhudumu katika fuo kama hizo, na hivyo kuwapotezea riziki. Kadhalika, jinsi ilivyotambuliwa katika tathmini ya kijamii, utata unaweza kuzuka pale ambapo shughuli za mradi zimeingilia misitu ya kaya za Mijikenda na maeneo takatifu kwa Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika, hivyo kusababisha kucheleweshwa au kuachwa kwa shughuli za miradi na hivyo kuwa na athari mbaya kwa jamii ambazo zililengwa kuboresha riziki zao katika kaunti za Kilifi na Kwale. Katika eneo la Lamu, hali ya ukosefu wa usalama na uhusiano kati ya wenyeji na jeshi la KDF unaweza kuwa ana athari mbaya kwa shughuli za mradi kwa jamii zinazoishi Lamu. Kwa sababu hiyo, Jamii za Saanye na Aweer zinaweza kuathirika kwa sababu ya uwezo wao wa kusafiri kudhibitiwa na tuhuma za kushirikiana au kuwaficha magaidi wa Al Shabaab katika misitu ya Boni na Witu. Kushauriana na Jamii 20. Fursa ya kwanza itakayoziwezesha jamii kutagusana na mradi, kutambua na kutathmini uzito wa athari mbaya utakuwa kupitia mashauriano. Mashauriano hayo yatafanywa ili kusanifu, kupanga na kutekeleza vipengele mbalimbali vya mradi wa KEMFSED na kutambua athari za mradi, zikiwemo nzuri na mbaya kwa jamii kwa kuzingatia mtazamo unaoshirikisha jamii. Ni muhimu sana kwa wawakilishi wa tabaka mbalimbali za jamii na hasa wavuvi, watambue umuhimu wa kushiriki katika mchakato huu. Watapewa fursa za kushiriki katika majadiliano yanayohusu usimamizi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mradi na kuanzishwa vya shughuli saidizi. Mashauriano ya wanajamii ndiyo itakuwa njia ya moja kwa moja kwa wanajamii kushiriki na kutoa mchango wao katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 10 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> mradi. Wakati wa mashauriano hayo, wanajamii wanaweza kuwatambua wale ambao wanaweza kuathiriwa kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali na wale ambao wanaweza kukosa katika utekelezaji wa shughuli za miradi ili muundo wa mradi uwezo kuangaliwa upya na kujumuisha wanajamii wote wa rika mbalimbali, jinsia, wenye ulemavu na wengine walio katika hatari ya kuathirika katika jamii. Kutakuwa na mwendelezo wa mashauriano na wanajamii na wavuvi ili kuzungumzia maoni yao kuhusu vikwazo vipya ili kutambua watumiaji walioathirika kimahususi. Kushirikiana na Mashirika Wakilishi 21. Kuna chama kipya kilichosajiliwa cha ushirika jijini Mombasa kinachoitwa Indian Ocean Water body kwa ajili ya jamii zote za wavuvi pwani. Chama hicho kinashirikisha shughuli za mtandao wa Vitengo vya Usimamizi wa Fuo katika eneo zima la Pwani huku kukiwa na mwenyekiti mkuu na wenyeviti wa mitandao ya kaunti. Pia kuna muungano wa Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika (VMG) Kilifi kwa ajili ya eneo zima la pwani. Lina mwenyekiti na uongozi unaoenda mpaka katika ngazi ya kijiji. Usajili wa muungano wa Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika katika Pwani ya Kenya ulifanikishwa na KCDP. KCDP ilitumia mtandao huu kuandaa na kutekeleza miradi kwa ajili ya Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika kwenye pwani ya Kenya. Mashirika wakilishi yatahusishwa kukiwa na uwakilishi unaozingatia jinsia ili yaweze kusaidia katika kuanisha athari za miradi kwa wanachama wao. 22. Wakati wa kutathmini matokeo, makini itaelekezwa kwa watu binafsi, nyumba na uhusiano wa kijamii pamoja na athari zinazotofautishwa kulingana na jinsia, hasa jinsi utekelezaji wa shughuli za mradi unavyoathiri uhusiano kati ya wanaume na wanawake. Wakati wa mashauriano, vitengo vya usimamizi wa mradi vitahusika katika kujadili njia mbalimbali za kuhakikisha kwamba walioathirika na mradi wanaweza kuepuka, kupunguza au kudhibiti athari zinazotokana na mradi. Kubaini Vigezo ya Kustahiki 23. Kitengo cha Kitaifa cha Utekelezaji wa Mradi (NPIU) kitafanya kazi kimsingi na Kitengo cha Kaunti cha Uratibu wa Mradi (CPCU) pamoja na mashirika ya maendeleo yanayoangazia jamii, mtandao wa vitengo vya usimamizi wa fuo na wahifadhi wa mazingira ili kufanikisha ushiriki wa jamii za wavuvi katika kubaini vigezo vya kustahiki. Kamati tendakazi iliyo na wawakilishi kutoka katika muungano wa vitengo vya usimamizi wa fuo, Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika kupitia vyama vya au vyama vya ushirika pamoja na vitengo vya utekelezaji wa mradi wa KEMFSED katika ngazi za kitaifa na kaunti zitaanzishwa ili kubuni mahitaji ya kustahiki kwa ajili ya usaidizi. Kigezo kitakachobuniwa sharti kiidhinishwe na Kamati Elekezi ya Mradi ya Kitaifa na Kaunti ambazo pia zinajumuisha wadau mbalimbali. Wale wanaostahiki kupata usaidizi ni Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 11 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> wanaoathiriwa moja kwa moja na shughuli za mradi kutokana na utumiaji na ufikiaji wa maeneo mbalimbali ya kutia nanga na bandari za uvuvi. 24. Utumiaji wa tangu jadi wa maeneo mahususi ya kutia nanga na bandari za uvuvi utazingatiwa wakati wa kuandaa vigezo vya kustahiki. UREJESHAJI NA USAIDIZI WA KUPATA RIZIKI 25. Kengo kuu la michakato ya kurejesha na kudhibiti ni kufidia na kuongeza mbinu zingine za kuchuma riziki kwa watumiaji wa bahari na rasilimali za samaki watakaoathiriwa na utekelezaji wa mradi wa KEMFSED. Mradi utasaidia kubuni biashara za ndogo na za kati katika jamii chini ya shughuli za kipengele cha 3 ambacho kitatoa kibadala cha uvuvi kwa kutoa fursa nyinginezo za riziki kwa wanajamii wanaoathirika. Mchakato wa kubuni biashara ndogo na za kati na mikakati ya riziki mbadala itakuwa shirikishi na itaongozwa na usawa katika juhudi za wanajamii kuongoza kufanya uamuzi. Uhamasishaji wa Jamii na Kurejesha Riziki 26. Wanajamii walioathiriwa watasaidiwa kuhamasishana ili kutambua shughuli mbadala za riziki wanazoweza kufanya kwa kushirikiana. Mtazamo huu utasaidia kuhakikisha kwamba kuna usawa katika mchakato na kwamba watumiaji wote walioathiriwa wakiwemo walio katika hatari ya kuathirika kwama vile wanawake, wazee na Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika, wana fursa ya kuhusishwa na kufaidika na usaidizi wa mbinu mbadala za kupata riziki zinazotolewa na mradi. Kuchukua mkondo huu kutazingatia mifumo inayokubalika kitamaduni ya kufanya uamuzi huku ukisaidia jamii za wavuvi wadogo wadogo kukuza uwezo wao wa kutathmini mahitaji yao na kuanzisha shughuli na suluhu katika ngazi ya jamii siku za usoni. Michakato ya Kufadhili Jamii 27. Miradi endelevu ya biashara katika jamii inayoandaliwa chini ya mradi mkuu itafadhiliwa kwa mpango wa ruzuku ndogo. Mpango huo utatoa rasilimali za kifedha kama mtaji wa awali wa uwekezaji katika biashara zinazoanzishwa. Ufanyakazi wa mpango wa ruzuku ndogo utazingatia mchakato uliowekwa. Kutokana na ukweli kwamba mipango ya usaidizi wa riziki na kwa walioahamishwa ni wa kurejesha hali ya kawaida, ruzuku haitatolewa kwa ushindani bali utawazingatia walioathirika zaidi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mradi wa KEMFSED. Endapo fedha zitabaki, fedha hizo zitatumiwa kufadhili miradi mingine ya jamii kama vile maji, uhifadhi wa mikoko na ulinzi wa maeneo yaliyotambuliwa ya kijamii/maeneo takatifu, utaratibu sawa sharti ufuatiliwe. Sehemu inayofuata inabainisha mpangilio wa mfumo na jinsi unavyotarajiwa kutekelezwa Fursa za Ajira Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 12 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> 28. Kutakuwa na fursa za ajira wakati wa utekelezaji wa mradi zitakazotumiwa kuwachukua baadhi ya wanajamii wanaohamishwa kutoka katika jamii za wavuvi, hasa pale ambapo ujuzi wao unalingana na kazi zinazohitajika. Wanajamii wenye ujuzi na wanaotaka wataajiriwa kwa kuzingatia uwezo ili watoe ujuzi wao wakati wa kutekeleza shughuli mbalimbali za mradi. Ujuzi unaohitajika utabainishwa mara baada ya shughuli za mradi kuratibiwa na kuidhinishwa. Jinsia na Masuala mengine ya Kijamii 29. Msisitizo maalum utawekwa katika usawa wa jinsia, kushiriki kwa watu wa asili na mashirika ya kijamii katika kuandaa na kutekeleza shughuli mbadala za kupata riziki. Wakati wa maandalizi ya KEMFSED, jamii za wenyeji zilishauriwa ili kubaini shughuli maalum na jamii zitakazosaidiwa. Ilitambuliwa kwamba wanawake wana jukumu kuu katika kuvuna maliasili ya baharini kupitia ushiriki wao moja kwa moja (kilimo cha mwani) na majukumu ya uzalishaji wa kijamii. Wanawake walihusika katika utoaji pamoja na uuzaji wa bidhaa za samaki (mama karanga). Kwa sababu hiyo, mradi utahakikisha kwamba wanawake wana fursa ya kushiriki na kutoa maoni kuhusu matarajio yao wenyewe wakati wa utambuzi na utekelezaji wa miradi midogo kwa ajili ya ufadhili. Masuala ya jinsia yanayoathiri ustawi wa familia za wavuvi au yanayokinza ushiriki wa wanawake yataangaliwa. Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika 30. Jamii za asili zilizotengwa na zilizo katika hatari ya kuathirika (Watha, Saanye, Aweer/Boni, Washiratzi, Watschwaka na Wakifundi) pia zitahusishwa kikamilifu ili kukuza ushiriki wao katika shughuli za mradi wa KEMFSED na katika kubuni mbinu mbadala zinazokubalika kitamaduni za kuchuma riziki. Miradi midogo inayokuza au kuhifadhi utamaduni wa Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika utazingatiwa ili kufadhiliwa palipo na uwezekano wa kiuchumi. Baadhi ya mapendekezo ya jamii za asili inajumuisha kuimarisha utalii wa kijamii na kimazingira unaojumuisha Waatha, lugha ya Wasaanye, mavazi ya jadi, vyakula vya kiasili au kuanzishwa kwa makundi ya burudani ya kitamaduni yatakayosaidia kupanua shughuli za kiuchumi miongoni mwa jamii za wenyeji. Kuhifadhi Misitu ya Kaya pamoja na maeneo mengine muhimu kwa kuabudu miongoni mwa Makundi Yaliyotengwa na Yaliyo katika Hatari ya Kuathirika kutatambuliwa na kuhifadhiwa ili kusaidia jamii kukuza turathi na shughuli za utalii wa kimazingira. Fursa hizi zitatoa manufaa yasiyo athari kwa jamii asili pale ambapo utamaduni wao utaangaziwa na kukuzwa huku wakiongeza mapato katika ngazi ya familia. Mashirika ya Kijamii 31. Jukumu na uhusika wa mashirika ya kijamii yakiwemo mashirika ya wavuvi na yale ya kuhifadhi mazingira utakuwa muhimu katika mradi huu katika kukuza miradi ya KEMFSED pamoja na katika kubuni mikakati mbadala ya riziki kwa jamii husika. Kuna mashirika Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 13 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> yaliyopo ya uhifadhi na vitengo vya usimamizi wa fukwe ambazo zimekuwa zikishirikiana na wenyeji kwa hivyo mradi huu utatumia uhusiano huo uliopo badala ya kubuni mifumo mipya katika jamii, isipokuwa ni muhimu kabisa. Majukumu ya Utekelezaji wa Mchakato wa Maendeleo 32. Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi (NPCU) na Kamati ya Kitaifa ya Uelekezaji wa Mradi (NPSC) zitahakikisha kwamba michakato ya maendeleo inatekelezwa na kufuatiliwa. Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi kitahakikisha utekelezaji wa shughuli za mradi wa KEMFSED na kina jukumu la kuandaa na kutekeleza mpangokazi wa mradi, kutekeleza mwongozo na bajeti pamoja na kusimamia rasilimali na wafanyakazi wasaidizi wa mradi. Kamati ya Ushauri wa Kiufundi katika Mradi (PTAC) katika ngazi ya kitaifa itasimamia utekelezaji wa sera, kanuni na michakato iliyoidhinishwa na Kamati ya Kitaifa ya Uelekezaji wa Mradi. Kamati ya Ushauri wa Kiufundi katika Mradi itashauriana na Idara ya Serikali ya Uvuvi, Kilimo cha Majini na Uchumi wa Rasilmali za Majini katika masuala ya usimamizi wa kifedha na amana. Pia itashauriana na Idara ya Uvuvi katika Taasisi ya Utafiti wa Bahari na Uvuvi ya Kenya (KEMFRI) katika masuala ya kiufundi, pamoja na washirika wengine wa KEMFSED katika utekelezaji. Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi kinawajibu na kutarajiwa kutoa ripoti za mara kwa mara kwa Kamati ya Kitaifa ya Uelekezaji wa Mradi kuhusu masuala yote ya shughuli za mradi. Wahusika wakuu wa masuala ya ulinzi wa kijamii wa Kamati ya Ushauri wa Kiufundi katika Mradi wana wajibu wa kutoa mwongozo wa kiufundi kwa miradi midogo iliyoidhinishwa chini ya kipengele vyote ikiwemo ufadhili chini ya miradi ya ufadhili unaolenga riziki. Wataalamu wa tatu wa ulinzi wa jamii wataajiriwa ili kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Mchakato wa Maendeleo na Mchakato wa Kutoa Makao Mapya katika kaunti za Kwale, Kilifi/Tana Delta na Lamu. Hili litahusisha kusimamia na kutoa mwongozo wa kiufundi katika mchakato wa kuomba na kuidhinishwa maombi yanayohusu miradi mbadala ya riziki. 33. Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi pia kina wajibu wa kufuatilia na kuthamini mchakato wa maendeleo. Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi itaripoti kwa Kamati ya Utekelezaji wa Mradi kuhusu shughuli zinazofanywa chini ya mchakato pamoja na masuala mengine ya utekelezaji wa mradi. Kamati ya Kitaifa ya Uelekezaji wa Mradi itatoa mwongozo wa jumla kuhusu utekelezaji wa vipengele vyote vya mradi wa KEMFSED. Inapohitajika, Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi kwa mashauriano na timu ya ulinzi wa maslahi ya kijamii ya Benki ya Dunia itawaajiri washauri wa kiufundi katika kufanya shughuli za mradi pale ambapo ujuzi kama huo wa kiufundi unahitajika, na iwe kibali kimepatikana kutoka katika Kamati ya Kitaifa ya Uelekezaji wa Mradi na isiwe imepingwa na Benki ya Dunia. Washauri pia wataajiriwa ili kusaidia jamii kuhamasishana na kushiriki katika upangaji wa kujihusisha. Katika hali zote kama hizo, Kamati ya Kitaifa ya Uelekezaji wa Mradi itatoa mwongozo na uangalizi wa kazi nyingine za mradi zinazofanywa na watu wengine. Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi pia itafanya kazi kwa ushirikiano na Idara Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 14 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> ya Uvuzi na timu ya ulinzi wa maslahi ya kijamii ya Benki ya Dunia pamoja na Kamati ya Ushauri wa Kiufundi katika Mradi katika masuala ya kiufundi katika mradi. Hili limefafanuliwa kwa kina hapa chini. Ushirikishaji wa Kiufundi 34. Kamati ya Ushauri wa Kiufundi katika Mradi na Idara ya Uvuvi zitafanya ushirikishaji wa kiufundi katika masuala yote ya utekelezaji wa shughuli za KEMFSED, utekelezaji wa kanuni za uvuzi na sehemu za kuzaliana. Washirika hawa wawili wa utekelezaji vitahusisha vitengo vya usimamizi wa fuo, idara husika za serikali za kaunti, jamii za wavuvi na wadau wengine katika mchakato wa mashauriano. Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi itatoa usaidizi wowote unaohitajika ili kufanikisha ushiriki wa wanajamii na itahakikisha kwamba mchakato wa maendeleo unafuatiliwa na vilevile ulinzi wa kijamii na mazingira umezingatiwa. Uratibu wa Ufadhili kwa ajili ya Mbinu Mbadala za Riziki 35. Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi kitashirikiana na Kitengo cha Kaunti cha Uelekezaji wa Mradi (CPCU) na Kamati ya Kaunti ya Ushauri wa Kiufundi (CTAC) katika utekelezaji wa mipango saidizi ya riziki mbadala kwa wanajamii walioathiriwa. Kamati ya Kaunti ya Uelekezaji wa Mradi (CPSC) itafuatilia shughuli za Kitengo cha Kaunti cha Uelekezaji wa Mradi (CPCU) na Kamati ya Kaunti ya Ushauri wa Kiufundi (CTAC) ili kuhakikisha kwamba zinazingatia Mchakato wa Maendeleo. Sababu kuu ni kwamba vitengo hivi vitatu vya utekelezaji katika kaunti viko katika ngazi ya mashinani na vinaweza kusaidia utekelezaji wa shughuli za mradi kwa urahisi. Hatimaye vitengo hivyo vitawasilisha ripoti kwa Kitengo cha Kitaifa cha Kuratibu Mradi ambayo hatimaye itaripoti kwa Kamati ya Kitaifa ya Uelekezaji wa Mradi. Kitengo cha Kaunti cha Uelekezaji wa Mradi (CPCU) pamoja na Kamati ya Kaunti ya Uelekezaji wa Mradi (CPSC) zitakuwa an jukumu la kufuatilia michakato inayohusika katika kusaidia jamii kupanga, kuandaa na kutekeleza miradi midogo. Washirika Wakuu wa Utekelezaji 36. Mradi wa KEMFSED utatekelezwa na Idara ya Serikali ya Uvuvi, Kilimo cha Majini na Uchumi wa Rasilmali za Majini ikiwa kiongozi kwa kushirikiana na idara mbalimbali za serikali kama vile za mimea, mifugo, uvuvi wizara ya Fedha, Idara ya Serikali ya Mazingira na Misitu, Mshirikishi wa baraza la pamoja la Sekta ya Kilimo katika ngazi mbalimbali za serikali, Muungano wa Vitengo vya Usimamizi wa Fuo katika Pwani (NCBMU), Muungano wa Wavuvi Pwani na Chama cha Wasindikaji na Wauzaji wa Samaki Kenya (AFIPEK) katika ngazi ya kitaifa; serikali za kaunti zinazopakana na ufuo zinazohusika zitatekeleza katika ngazi ya kaunti. Zitatoa mbinu za ufuatiliaji na utekelezaji katika kiwango cha kaunti. Chini ya viwango vya kaunti vya utekelezaji na viwango vya usimamizi, kutakuwa na Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 15 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> viwango vya jamii vya miundo ya utekelezaji ambavyo vitajumuisha hasa Mashirika ya Maendeleo Yanayosimamiwa na Jamii (CDDO). Miundo ya utekelezaji katika kiwango cha jamii itakuwa na kamati ndogo. Mifumo ya Kufuatilia ya Malalamiko 37. Malalamiko na migogoro inaweza kutokea katika ngazi mbalimbali za upangaji na utekelezaji wa Mradi na inaweza kuhusiana na usimamizi wa mradi au unaweza kutokana na migogoro kati ya makundi yaliyoathiriwa na Mradi. Makundi na watu wote wanaoathiriwa ilivyofafanuliwa kwenye Mradi sharti wafahamishwe katika kila hatua kwamba kuna mchakato wa kusuluhisha malalamiko na washauri jinsi ya wanavyoweza kutumia mfumo huo. 38. Kwa mtazamo wa Mfumo wa Kufuatilia Malalamiko katika mradi huu, lalamiko ni suala, dukuduku, tatizo au dai (la kudhani au la kweli) au malalamiko ambayo mtu au kundi linataka mradi lishughulikie au kutatua. Inaeleweka kwamba wanajamii wanapowasilisha malalamiko, kwa kawaida huwa wanatarajia mojawapo ya yafuatayo: a) Kutambuliwa kwa tatizo lao b) Jibu la kweli kuhusu swali walilo nalo kuhusu shughuli za mradi c) Kumbwa msamaha d) Fidia e) Kubadilishwa kwa jambo lililosababisha lalamiko f) Suluhisho lingine la haki. 39. Mfumo wa kufuatilia malalamiko utaandaliwa ili kushughulikia aina nne za malalamiko yanayoweza kutokea ambazo ni: a)Maoni, mapendekezo au maswali; b)Malalamiko yanayohusu kutotekeleka kwa malengo ya mradi; c)Malalamiko yanayohusu ukiukaji wa sheria na/au ufisadi; na d)d) Malalamiko dhidi ya wafanyakazi wa mradi au wanajamii wanaohusika katika usimamizi wa mradi. Lengo na Wigo wa Mchakato wa Ufuatiliaji na Tathmini 40. Lengo la mchakato wa maendeleo katika mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ni kufuatilia upana na ukubwa wa athari mbaya na ufaafu wa mbinu zilizobuniwa ili kuwasaidia watu walihamishwa kuboresha na kurejesha mbinu za kupata riziki na mapato. Inatarajiwa kwamba wadau, hasa wa jamii za wavuvi ambao wanaweza kuathiriwa na utekelezaji wa shughuli za mradi wa KEMFSED kwa kiasi fulani kutokana na kuanzishwa kwa kanuni mpya au kutekelezwa kwa kanuni zilizopo kwa kuwepo kwa mifumo mipya ya usimamizi, udhibiti wa uvuvi unaopitiliza, kudumisha idadi ya samaki na kufanya maeneo ya kutia nanga na bandari za samaki kuwa za kisasa watashiriki kikamilifu katika mchakato wa Ufuatiliaji na Tathmini. Wale ambao wananufaika kutokana na usaidizi wa kurejesha mbinu Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 16 << MCHAKATO WA MAENDELEO >> za riziki pamoja na mbinu za udhibiti wa athari watahitajika kufuatilia na kutathmini ubora wa mifumo mbadala inayotekelezwa chini ya mradi huu. Mradi wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii na Uvuvi wa Baharini nchini Kenya(KEMFSED) 17