E2525 v7 MAPENDEKEZO YA UKARABATI NA UBORESHAJI WA BARABARA YA MIZINGANI KATI YA BUSTANI YA FORODHANI NA ENEO DURA LA MTI WA BANIANI UTATHMINI WA ATHARI YA KIJAMII NA KIMAZINGIRA Muhtasari wa Usimamizi 1 1 UTANGULIZI Mamlaka ya Maendeleo na Uhifadhi wa mji mkongwe (STCDA) inapendekeza kukarabatiwa na kuboreshwa kwa kijisehemu cha Barabara ya Mizingani katika sehemu ya mbele ya bahari ya Mji Mkongwe wa Zanzibar. Mradi wa uboreshaji wa sehemu ya mbele ya bahari ya Mizingani unajumuisha sehemu ya mradi wa huduma za mijini zanzibar (ZUSP) katika utekelezaji chini ya mkataba wa Benki ya Dunia na Serikali ya ya Mapinduzi ya Zanzibar (RGZ). Msaada wa kiufundi wa mradi uliotajwa hapo juu unatolewa kwa STCDA na Wakf wa Utamaduni wa Aga Khan (AKTC). Aurecon imeteuliwa kuwa mshauri wa kujitegemea wa kimazingira katika kutathmini athari ya Kijamii na Kimazingira (ESIA) na Usimamizi wa Mpango wa Kijamii na Kimazingira katika ukarabati huu uliopendekezwa wa ukuta wa kuzuia maji ya bahari wa Mizingani na barabara yake. Lengo kuu la ESIA ni kutambua, kufafanua, kutabiri, kutathmini na kujumlisha athari, vizuizi na hatari ili kutaarifu RGZ, AKTC na Benki kuu ya Dunia kuhusu vikwazo vya kijamii na kimazingira na wasiwasi wa umma unaohusiana na mradi huu husika pamoja na mseto wa hatua za uboreshaji zilizopo. ESIA inatoa tathmini ya pamoja katika maswala ya kimazingira yanayohusiana na maendeleo yanayopendekezwa. Athari hizi zinatokana na michango mbalimbali ya mijadala iliyofikiwa kutokana na mwitikio wa michango kwa kuwashirikisha washikadau, mamlaka husika na kundi la wataalamu wa Kutathmini Athari za Kijamii na Mazingira (ESIA) Muhtasari wa mchakato huu wa ESIA pamoja na matokeo yake umetolewa katika muhtasari huu wa watendaji. 2 Mandhari ya Barabara ya Mizingani kutoka katika jengo la Forodha la zamani (Old Customs house) ukielekea kwenye mkahawa wa Mercury 3 1.1 UFAFANUZI WA MRADI Mradi huu uliopendekezwa unajumuisha shughuli zifuatazo: i. Ujenzi wa ukuta wa kuzuia maji ya bahari ulio na urefu wa takriban mita 315, uwezekano wa ardhi iliyoboreshwa ipatayo mita 5 kutoka katika kimo cha sasa, ikijumuisha ujalizaji ufaao pamoja na kazi ya uwekaji msingi; ii. Ukarabati wa miundo mbinu ya chini kwa chini ikiwemo maji, majitaka na dhoruba. Hivi vyote vitakuwepo chini ya sakafu ya chini ya Barabara ya Mizingani, iii. Ukarabati wa barabara na uanzilishwaji wa maswala ya usalama na upunguzwaji wa msongamano wa magari na pia wapita njia. Barabara hii itakuwa na upana wa kutosha kutoa njia mbili za kupishana magari, maegesho, sambamba na kijia kidogo kando ya majengo kwa waendao kwa miguu ( takriban mita 6-7 ); na iv. Uwezekano wa kuanzisha sehemu ya matembezi ya waendao kwa miguu ambayo itakuwa mita 5.8 kwa upana pamoja na uwekaji wa taa za barabarani na mapambo kando kando ya ukuta upande wa baharini. Sehemu ya Barabara ya Mizingani iliyo kusudiwa katika mapendekezo haya ya maendeleo inaanzia mkahawa wa Mercury mkabala na eneo la mti wa Kibaniani hadi mwisho kwenye ngazi za kushukia Sultan katika Bustani ya Forodhani. Ramani ya eneo hili, mahali pa mradi pameonyeshwa 1.2 MBINU Tunazo awamu tatu kuu katika mchakato wa ESIA, kama inavyohitajika katika kanuni za Kifungu cha Sheria cha Maendeleo ya Uendelevu ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (EMSDA) (Nambari 2 ya1996), awamu hizi ni kama vile kwanza kuwasilisha maombi, Ripoti ya Upeo na Ripoti ya Utathmini. Ripoti hii inajumuisha awamu ya pili na ya tatu, dhidi ya awamu za upeo na utathmini. 4 Awamu ya kwanza: Masharti/Kanuni za Rejea Itaidhinishwa na Idara ya Mazingira kulingana na Usimamizi Endelevu wa Kimazingira wa Kifungu cha Sheria ya Maendeleo Endelevu mwaka wa 1996 Awamu ya 2: Awamu ya Upeo Utambulisho na uchunguzi wa athari inayowezekana Awamu ya 3: Tathmini ya Utathmini wa athari unatambuliwa wakati Athari wa awamu wa Upeo Kuwasilisha Katika Idara ya Mazingira Ufichuzi kwa Umma Inatekelezwa na Idara ya Mazingira Awamu ya Utoaji Maamuzi Mchoro wa mchakato wa Utathmini wa Athari wa Kimazingira Zanzibari 1.2.1 Awamu ya Upeo Awamu ya upeo inafafanuliwa kuwa utaratibu wa kuamua kutambua kiwango na mtazamo wa utathmini wa kimazingira na kijamii na inajumuisha kazi kuu zifuatazo: · Ushauriano na washikadau wanaohusika; · Utambulisho na uchunguzi wa njia mbadala; · Utambulisho wa maswala muhimu ya kuchunguzwa katika Ripoti ya Athari ya Kimazingira na kijamii (ESIR); na · Maamuzi ya mbinu kwa ajili ya ESIR 5 Utembeleaji wa awamu hii ya Upeo kwenye eneo lenyewe la kazi ulitekelezwa kutoka tarehe 13 Machi 2010 hadi 31 machi 2010 wakati ambapo eneo la kufanyiwa utafiti na mazingira lilitembelewa na washikadau walihusishwa ipasavyo. 1.2.2 Utathmini Awamu ya utathmini inajumuisha kiungo cha mwisho cha ESIA kabla ya uwasilishwaji katika taasisi inayohusika na mazingira. Kusudio la ESIA ni kufafanua na kutathmini aina mbalimbali ya uwezekano mbadala unaoweza kutokea ambao utatambuliwa wakati wa mchakato wa Upeo kulingana na uwezekano wa athari za kimazingira zilizotambuliwa. Mbinu za awamu ya Upeo ESIR unajumuisha yafuatayo: · Kutekeleza mapitio ya ziada ya fasihi ifaayo; · Uteuzi wa wataalam mbalimbali wa kutekeleza utafiti wa kitaalam uliotambuliwa wakati wa awamu ya Upeo, · Utekelezaji wa kutembelea tena eneo hilo kutoka mnamo tarehe 14 hadi 24 Aprili mwaka wa 2010. Kushauriana na wadau kulianzisha sehemu muhimu ya uchunguzi huu na ikawezesha wadau kutoa maoni juu ya uwezekano wa athari za mazingira yanayohusiana na njia mbadala za kufanya upembuzi yakinifu na kubaini masuala ya ziada ambayo wao walihisi hayakushughulikiwa vya kutosha katika awamu ya Upeo. Hatimaye, msingi wa tathmini ya ESIR, imejumisha hatua zilizoundwa kukabiliana na maboresho yanostahiki na athari zinazohusiana kutathminiwa upya kwa ufanisi na uchambuzi linganishi 1.3 AWAMU YA UPEO Vipengele vifuatavyo vilitekelezwa kama sehemu ya awamu ya Upeo ya ESIR. 1.3.1 Uhushirikishwaji wa Washikadau katika Upeo. Washikadau waliulizwa kwa kutumia njia tatu tofauti. Hii ilikuwa mahojiano juu ya taarifa mahususi, majadiliano ya vikundi na mikutano ya pamoja na washikadau. Washikadau mbalimbali walijumuishwa wakiwemo maofisa wa kiserikali, wamiliki wa ardhi, wapangaji, waendesha mashua, wavuvi, wafanyibiashara rasmi na wasiokuwa rasmi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Wasiwasi na matarajio kuhusu mradi unaopendekezwa na matokeo ya athari zake katika muundo wa mradi, hatua za kukabiliana na hatua za kuchukuliwa katika hatua mbali mbali zinazofuata za athari ya utathimini yalizungumzwa. Ingawaje malamiko mengi pamoja na mambo mbalimbali yalizungumziwa, swala kuu lilikuwa ni kuhusiana na mzunguko mzima wa mradi wakati wa ujenzi na kupata kuutumia ufuo wa pwani kwa shughuli za kazi zao, ambao hutumiwa na waendesha 6 maboti, wafanyibiashara wasiokuwa rasmi na wauzaji bidhaa. Vilevile, lalamiko kuhusiana na mitetemeko wakati wa awamu ya ujenzi pamoja na athari zake katika majengo yaliyo karibu liliweza kuzungumzwa kuwa ni kama suwala nyeti. Pia imezungumziwa na wadau wasiwasi wa uwezekano juu ya hisia ya mradi huu pendekezwa kuwa utakuwa ni "chachu" ya maendeleo kwa uboreshaji wake wa ardhi. 1.3.2 Njia Mbadala Maendeleo na kutambua njia mbadala ni michakato usioisha ya uchunguzi na kushauriana wakati ambapo maeneo mbadala, teknolojia, au shughuli zilizoainishwa katika mazingira ya mradi ulio pendekezwa. Kama ilivyo upeo wa mahali pa kufanyiwa kazi na njia mbadala ya teknolojia ni kidogo, lengo lilikuwa na njia mbadala za utendaji, yani, maumbo mbalimbali na viwango ambavyo mradi pendekezwa ungechukua. Mibadala ifuatayo ilitambuliwa: 1. Hali Kama Ilivyo/ Chaguo la-Kutotumia, hili ni chaguo la kutofanya chochote na kuuacha ukuta wa kuzuia maji ya bahari ya Mizingani na miundo mbinu husika kama ilivyo; 2. Ubadilishaji wa ukuta wima, ujenzi wa Ukuta wa kuzuia maji ya bahari katika mahali ulipo hivi sasa; 3. Ubadili wa mawe ya ukingo, ujenzi wa Ukuta wa kuzuia maji ya bahari uliopo kama mawe ya ukingo (Ukuta wa kuzuia maji ya bahari unaojiinamia) katika mahali ulipo hivi punde; 4. Sehemu wima ya matembezi, Huu ni ubadilishaji wa sehemu ya mbele ya bahari ipatayo takribani mita 5, ujenzi wa ukuta unaokaribia wima wenye masi mvutano na wenye maendeleo ya Matembezi yapatayo mita 5.8 na miundo mbinu husika; 5. Sehemu ya matembezi ya mawe ya ukingo, huu ni ubadilishaji wa mbele ya bahari upatao takribani mita 5, ujenzi wa mawe ya ukingo, maendeleo ya Matembezi yapatayo mita 5.8 na miundo mbinu husika; 6. Sehemu nyembamba ya matembezi ya mawe ya ukingo, maendeleo ya ukuta wa mawe ya ukingo ukihusika na ubadilishaji wa takribani mita 5, ujenzi wa Sehemu ya Matembezi ipatayo mita 5.8 kutoka Bustani ya Forodhani hadi kwenye hatua za kituo cha Mizingani ambapo mawe ya ukingo yatapangiliwa upya na mpagilio wa ukuta uliopo mpaka kwenye Mkahawa wa Mercury ; na 7 7. Sehemu wima na nyembamba ya matembezi , maendeleo ya ukuta wima wa masi mvutano ulio karibu kwa kuhusishwa na ubadilishaji wa takribani mita 5, ujenzi wa sehemu ya Matembezi mita ipatayo 5.8 kutoka Bustani ya Forodhani hadi katika hatua za kituo cha Mizingani ambapo mawe ya ukingo yatapangiliwa upya na mpangilio wa ukuta uliopo mpaka katika Mkahawa wa Mercury 1.3.3 Uchunguzi Njia mbadala zilizotajwa hapo juu iliangaliwa kwa mujibu wa maswala yafuatayo: · Vifaa vya ujenzi, mbadala wa mwasi uliopo, yani tambara tumbawe, chokaamawe, mawe ya saruji nk,; · Utangulizi wa kihistoria, kulingana na matukio yaliyopita ya ukuta wa kuzuia maji ya bahari hiyo na hali nyingine za ulinzi wa ufuo; · Uboreshaji wa mmomonyoko wa udongo, uwezekano na matokeo ya mmomonyoko wa udongo kutokana na mibadala mbalimbali hususan utofauti kati ya ukuta wa masi mvutano na mawe ya ukingo; · Uzidishaji, athari na uwezekano wa umwagikaji wa maji ya bahari kwenye kiliele na kileleta cha ukuta; · Nyayo, kiwango cha nyayo za mibadala mbalimbali; na · Matumizi, matumizi ya jamii ya jengo lililoko hivi sasa pamoja na uwezekano wa kutumia jengo jipya. Kwa mujibu wa mazungumzo ya kina kuuhusu utaratibu uliotajwa hapo juu, nji mbadala mbalimbali ziliweza kuchunguzwa na hatimaye yafuatayo yalisukumwa mbele hadi katika awamu ya utathmini: · Hakuna kwenda mbadala · Njia Mbadala ya 1: Njia Mbadala ya ubadilishaji ukuta wima · Njia Mbadala ya 2: Njia Mbadala ya sehemu ya matembezi wima; na · Njia Mbadala ya 3: Njia Mbadala ya Sehemu nyembamba ya Matembezi wima. 8 SEHEMU YA MBELE YA BAHARI YA MIZINGANI ZANZIBARI - MPANGO WA USANIFU WA EIA-CHAGUO LA 1 Mbadala 1: Ubadilishaji wa ukuta wima 9 Mbadala 2: Sehemu Wima ya Matembezi 10 Mbadala 3: Sehemu wima na nyembamba ya matembezi 11 1.4 AWAMU YA ATHARI YA UTATHMINI Baada ya kutoka awamu ya upeo ya tathmini ya athari zaidi inahusu madhara ya kutambuliwa katika upeo, Tathmini ya athari hizo, na kuishia kwenye muhtasari uliopatikana kutokana na tathmini hii. 1.4.1 Ushauri wa washikadau Ushauri wa washikadau wakati wa awamu ya athari ya utathmini unajumuisha mahojiano na wahusika wakuu na mazungumzo na kundi lengwa. Maoni yafuatayo na malalamiko yalitolewa na washikadau ambao walishauriwa wakati wa shughuli hii ya wakati wa utathmini. · Suala lililotolewa kuhusu msongamano mwingi na maegesho katika awamu ya ujenzi; · Suala la kuhusu ufikivu wa hadi katika majengo yaliyopo kando ya eneo la mradi wakati wa ujenzi; · Uwezekano wa uharibifu wa makaburi kwenye maziara ya kasri; · Msaada kwa biashara za hapo huenda hautaathiriwa na ujenzi na utafaidi kutokana na uendeshaji huu; · Suala la kuhusu matumizi ya sehemu ya mti baniani baada ya mradi kukamika; · Suala la kuhusu kuto ruhusiwa kufanya biashara kweye njia katika Barabara ya Mizingani, pamoja na kwamba vizuizi kama hivyo katika Bustani ya Forodhani vitatekelezwa; · Upotezaji wa eneo la ufuo (ukubwa utapungua) · Suala la kuhusu mahitaji ya leseni ya kufanyia kazi katika eneo la mradi; · Suala la kuhusu kuzuiliwa kwa matumizi ya sehemu fulani za mradi huo ulioboreshwa; · Suala la kuhusu matumizi ya changarawe kwa kusudio la ujenzi na hivyo basi kusababisha kuharibika kwa ufuo; · Uwezekano wa kuharibika kwa haki za kuwa na bandari katika ufuo wa Mizingani; · Suala la kuhusu kuajiriwa kwa wenyeji katika awamu ya ujenzi; na · Suala la kuhusu usafirishwaji wa watoto wa shule wa eneo hilo wakati wa awamu ya ujenzi. Maswala na malalamiko yaliyotolewa yalifungamanishwa katika utathmini wa athari zilizotambuliwa na hatua za uboreshaji kwa kuyazingatia hayo yaliyotajwa hapo juu, na kukubalika, yaliyo pendekezwa yote. 1.4.2 Mabadiliko ya usanifu Kutokana na uchunguzi na mabadiliko katika ushirikishwaji wa washikadau katika usanifu uliopendelezwa, viliweza kupendekezwa. 12 Mabadiliko haya yalilenga katika kuangazia baadhi ya maswala na malalamiko yaliyotolewa na washikadau pamoja na timu ya mradi pamoja na kuzungumziwa kwa faida zinazowezekana kutoka katika mtazamo wa mpangilio. Usanifu una mitazamo miwili. · Machaguo ya usanifu yanayohusishwa na vidaraja vya Ukuta wa kuzuia maji ya bahari kuelekea katika vidaraja vilivyopo kando ya Mkahawa wa Mercury; na · Mabadiliko katika visehemu na viwango vya mbadala vya sehemu ya matembezi wima Iliyojiinamia 13 Mabadiliko ya Usanifu wa Vidaraja 1. Mabadiliko ya 1 ya Vidaraja vya Ufuo - Kama mpango asilia wa vidaraja vimewekwa kwenye sehemu ya matembezi na vinaishia katika kwa mstari moja na ukuta wa kuzuia maji ya bahari. Hata hivyo chelezo cha mashua imeongezewa kwenye ngazi ili kurahisisha ufukivu kutoka kwenye ufuo kwenda kwenye ujenzi au utengenezwaji wa mashuawa chini ya Mti wa Kibaniani. 2. Mabadiliko ya 2 ya vidaraja vya ufuo ­ chaguo la vigazi hivi vinaanzia ukingoni mwa ukuta wa kuzuia maji ya bahari na kuelekea chini hadi kwenye ufuo. Hakuna mkatizo kwenye sehemu ya njia ya miguu. Na pia chelezo cha mashua kimewekwa katikati. 3. Mabadiliko ya 3 ya vidaraja vya ufuo - Chaguo hili yamkini ni sawa na chaguo la kwanza, linajumuisha chelezo cha mashua lakini vigazi ni virefu zaidi na vinarefuka zaidi kando kando ya urefu wa sehemu ya matembezi. 1 2 3 Mitawanyo ya vigazi vya ufuo Upana wa Mabadiliko 1. Upana tofauti wa 1: Njia Mbadala ya Sehemu asilia ya njia ya miguu. Sehemu ya Matembezi ipatayo mita 5.8, barabara pana ya mita 7, eneo la maegesho la mita 2.5 na sehemu ya kutembelea yenye upana unaotofautiana.Ubadilishaji wa ardhi katika chaguo hili ni mita 5 2. Upana tofauti wa 2: Sehemu ya Matembezi Ipatayo mita 5.8, barabara pana ya mita 6, eneo la maegesho lipatalo mita 2.5, na sehemu ya pembeni ya wapitao kwa miguu yenye upana unaotofautiana. Ubadilishaji wa ardhi katika chaguo hili ni mita 4, ya upana, 3. Upana tofauti wa 3: Sehemu ya wapitao kwa miguu ipatayo mita 5.8, barabara pana ipatayo 6.6, eneo la maegesho lipatalo mita 2.6 na sehemu ya 14 MPANGO WA UPANA CHAGUO LA 1 MPANGO WA UPANA WA BARABARA CHAGUO LA 2 MPANGO WA UPANA WA BARABARA CHAGUO LA 3 Mabadiliko ya upana 15 pembeni ya wapitao kwa miguu yenye upana unaotofautiana lakini ulio mkubwa zaidi kuliko njia mbadala zile bili. Ubadilishaji wa ardhi katika chaguo hili ni mita 5. Ingawaje mabadiliko haya ya usanifu hayakuwepo wakati wa kukutana na washikadau, maoni ya kila mmoja yalijumuishwa kwenye athari ya utathmini kama ilivyostahiki. 1.4.3 Utathmini Sehemu hii ya ESIR inatoa ufafanuzi wenye maelezo zaidi kuhusu uwezekano wa athari kama zinavyojihusisha katika maendeleo yaliyopendekezwa ya ukarabati wa Barabara ya Mizingani na uboreshaji wake ambao huenda utafanyika kutokana na utekelezaji wa njia mbadala iliyopendekezwa. Athari hizi zimekuwa kwa mujibu wa tathmini wenye maelezo zaidi na inajumuisha uwezekano wa athari za kibaiolojia na maumbile na kiuchumi na jamii ambazo zinaweza kutokea kutokana na wakati wa awamu ya uendeshaji. (yaani athari za muda-mrefu) na awamu ya ujenzi (yani athari za muda-mfupi) kwa shughuli zilizopendekezwa. Jedwali la 2 linatoa kiini cha majedwali ya tathmini yaliyotolewa hapo chini. Jedwali 2. Mukhatasari wa alama za rangi huku zikiashiria na kumaanisha umuhimu wa athari mbalimbali Asi kuu Nyekundu Asi wastani Chungwa Asi chini Njano Asi Chini Zaidi Kijani Isobadilika/Hapajaziki Nyeupe Athari ya Chanya Chini Samawati Athari ya Chanya Chini Lilaki Athari ya Chanya Waridi Athari ya Chanya Juu Balungi Kwa mujibu wa makundi ya Athari zilizotambuliwa wakati wa upeo athari zilizoko katika Jedwali la 3 zilitolewa humo na hatimae kutathminiwa. Table 3: Construction and operational phase impacts assessed during the impact assessment phase. Jedwali 3: Ujenzi na athari za uendeshaji tathmini ilitofanywa katika kipindi cha awamu ya tathmini ya athari. 16 Jedwali la 3: Aina ya athari · Upatikanaji wa kazi wakati wa ujenzi · Ongezeko la masoko kwa wajasiriamali wa nchini · Ongezeko kuathiri uchumi wa jamii na wa kitaifa · Uwezekano wa uhamishwaji muda wa makazi kiuchumi · Kumiminika kwa watafutaji kazi · Kupoteza au kupunguza matumizi ya katika ufuo · Ukatizaji wa eneo la baina ya maji kupwa · Ujenzi wa kuzalisha uchafu Ujenzi · Kelele na uchafuzi wa hewa (vumbi) · Mitetemeko · Uwezekano wa kuhisi kuondolewa mahali kwa muda · Rasilimali za urithi · Kuzuiliwa kulitumia eneo la katika mti wa Kibaniani · Kuzuiliwa kwa watembea kwa miguu · Usumbufu wa mzunguko na msongamano · Kuzuiliwa katika maegesho · Ukatizaji wa huduma za miundo mbinu · Upatikanaji wa kazi wakati wa ujenzi · Fursa za biashara kwa wajasiriamali wa eneo hilo · Ustawishaji wa usalama kwa wendao kwa miguu na misongamano · Ukubwa na mzunguko wa msongamano · Kungezeka kwa majivuno ya kiraia · Rasilimali za kitamaduni na urithi na hali ya WHS · Ubora wa nafasi ya wazi · Ongezeko la miti ya minazi · Ongezeko la taa za barabarani na samani · Utoaji huduma Uendeshaji · Uwezekano wa kubadilishwa kwa kudumu kiuchumi · Kupoteza au kupunguza matumizi ya katika ufuo · Mabadiliko ya kimo cha ukuta wa kuzuia maji ya bahari (upana na urefu) · Mmomonyoko wa udongo mnyevumnyevu katika vifaa vya ujenzi · Makazi ya asili ya ukuta wa kuzuia maji ya bahari · Eneo la baina ya maji kupwa · Kuzuia mmomonyoko na ufungiaji wa chenga 17 1.4.4 Athari za awamu ya ujenzi Athari za awamu ya ujenzi, kama zilivyoonyeshwa katika Jedwali la 3 hapo juu, zilitathminiwa kwa mujibu wa kipindi, kiwango, wingi na uwezekano wa kutambua ukubwa wa athari hizo zilizopendekezwa pamoja na umuhimu wake. Kati ya athari za awamu ya ujenzi zilizotajwa, hakuna zile zilizoonekana kwamba zinayo athari kubwa zaidi katika mazingira (Kibaolojia ya kimaumbile na kijamii), ukichukulia kiwango chao cha kipindi kifupi kwa kiasi fulani na katika eneo dogo. Wingi wa athari za awamu ya ujenzi ni za umuhimu mdogo, utekelezaji wa mwingiliano wa mkusanyiko wa uboreshaji kama ilivyofafanuliwa kwenye Mpango wa Usimamizi wa Kijamii na Kimazingira (ESMP) unachukuliwa kuwa mwafaka. 18 Jedwali 4: Muhtasari wa jedwali la umuhimu wa athari za awamu ya ujenzi Mbadala wa 1- Ubadilishaji wa Ukuta Mbadala wa 2- Sehemu Wima ya Mbadala wa 3- Sehemu Wima na Wima Matembezi Nyembamba ya Matembezi Athari Na Bila ya Bila ya Na Bila ya Na uboreshwaji uboreshwaji Uboreshwaji uboreshwaji uboreshwaji uboreshwaji ATHARI ZA AWAMU YA UJENZI CHINI (+) Upatikanaji wa ajira wakati wa shghuli za WASTANI(+) CHINI (+) WASTANI(+) CHINI (+) WASTANI(+) Yawezekana ujenzi Yawezekana Sana Yawezekana Kiasi. Yawezekana Sana Yawezekana Kiasi Yawezekana Sana Kiasi CHINI (+) Ongezeko la masoko kwa wajasiriamali wa LOW (+) CHINI SANA (+) CHINI (+) CHINI SANA (+) CHINI (+) Yawezekana nchini Yawezekana Sana Yawezekana Kiasi Yawezekana Sana Yawezekana Kiasi Yawezekana Sana Sana Ongezeko kuathiri uchumi wa jamii na wa CHINI (+) CHINI (+) CHINI (+) CHINI (+) CHINI (+) CHINI (+) kitaifa Yawezekana Yawezekana Sana Yawezekana Kiasi Yawezekana Sana Yawezekana Kiasi Yawezekana Sana Kiasi CHINI (-) Uwezekano wa uhamishwaji wa muda wa CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) Yawezekana kiuchumi Haiwezekani Hakika Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Kiasi Sana CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) Kumiminika kwa watafutaji kazi Yawezekana Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Kiasi Kupoteza au kupunguza matumizi ya katika CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) ufukwe Yawezekana Yawezekana Kiasi Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Sana CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) Ukatizaji wa eneo la baina ya maji kupwa Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) Ujenzi unaofanyizwa katika eneo lililovurugika Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika Kelele na uchafuzi wa hewa (vumbi) CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika WASTANI (-) CHINI (-) WASTANI (-) CHINI (-) WASTANI (-) CHINI (-) Mtetemeko Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Yawezekana Kiasi Uwezekano wa kuhisi kuondolewa mahali kwa CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) muda Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) Rasilimali za urithi Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Kuzuiliwa kulitumia eneo la katika mti wa CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) Kibaniani Yawezekana Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Kiasi Kuzuiliwa kwa watembea kwa miguu CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana 19 WASTANI(-) WASTANI(-) CHINI (-) CHINI (-) WASTANI (-) WASTANI (-) Usumbufu wa mzunguko na msongamano Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) Kuzuiliwa katika maegesho Yawezekana Yawezekana Kiasi Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Sana CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI SANA (-) Ukatizaji wa huduma za miundo mbinu Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Yawezekana Kiasi 20 1.4.5 Athari za Uendeshaji Awamu ya athari za uendeshaji ilikuwa ikionyesha kutafakari kwamba kuna faida kubwa ya kijamii na ya maendeleo ya njia ya waendao kwa miguu. Athari za awamu ya uendeshaji zilionyeshwa kutafakari kwamba kuna faida kuu kubwa ya kijamii na katika maendeleo ya njia ya waendao kwa miguu.Uwezekano wa athari zilizotambuliwa kuwa mwafaka katika awamu hii ya uendeshaji katika mradi huu zimeorodheshwa katika Jedwali 3 na vipimo vya umuhimu wake kutolewa kwa muhtasari wake katika Jedwali 5 hapa chini Kitamaduni Umuhimu wa kitamaduni wa Barabara ya Mizingani kwa mujibu wa ufundi sanifu na historia unatiliwa maanani na umuhimu wake wa kipekee katika kuwa sehemu teule na kiingilio katika kisiwa. Hivyo basi ni muhimu barabara hii ikiwa ndio uso wa umma wa taifa la Zanzibari (Attwell, 2010). Athari za urithi zilitathminiwa kuwa bora isipokuwa tu uwezekano wa mmomonyoko wa udongo mnyevunyevu unaosababishwa na sehemu zilizokauka dhidi ya ukuta wa mbele wa jengo. Muhtasari uliofikiwa na wataalam wa urithi ni kwamba uboreshaji wa Barabara ya Mizingani, ambao unaenda sambaba na Mpango ulioidhinishwa wa Majadiliano, huenda ukawa na athari ya kuongezeka katika rasilimali za urithi na ukafikia uboreshwaji wa kimajengo na kirejeshi kama matokeo yake. Hivyo basi athari kwenye rasilimali za urithi au kitamaduni huenda ikawa chache sana na ndani ya viwango vinavyokubalika vya mabadiliko katika sehemu ya urithi ulimwenguni. Hivyo basi inaonekana kuunga mkono jitihada za uhifadhi wa Mji Mkongwe zinazoendelea. Athari ya kijamii-kiuchumi Ni wazi kwamba uwezekano wa faida za kijamii unakuja kwa gharama ya mazingira ya kimaumbile hata hivyo katika mazingira ya baharini zimo ndani ya viwango vinavyokubalika kwa maana eneo hilo la baina ya maji kupwa litapitia athari ya kipindi kirefu kilicho na mipaka pamoja na kwamba hazitakuwa na athari zozote za kutambulika katika ufukwe kama inavyotarajiwa. Faida za kijamii zinaanzia katika majivuno ya umma yaliyoboreshwa hadi katika mzunguko ulioboreshwa wa msongamano na usalama wa wendao kwa miguu huku faida za kiuchumi zikijumuisha fursa za biashara kwa wajasiriamali na kuongezeka kwa ajira. Athari za kiekolojia Mazingira ya bahari kando ya sehemu husika yameathiriwa pakubwa na mwingiliano wa kianthropojenia katika kando ya sehemu husika ya kujumuishwa pia na ulinzi wa Bustani ya Forodhani na Bandari. Upotezwaji wa makazi ya asili ya mita 5 katika eneo la pwani la baina ya maji kupwa unatarajiwa kubadilishwa kwa kiasi kikubwa na tambara tumbawe litakalotumiwa 21 katika msingi wa ujenzi huu mpya na uhamaji wa mchanga katika kipindi kifupi na cha wastani kijacho. Ufukwe unadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na muundo wa Bandari na kwa hivyo haitarajiwi kwamba utaweza kupata zaidi ya athari asi ya kiwango cha chini. 22 Jedwali la 5: Muhtasari wa jedwali kuhusu umuhimu wa athari katika awamu ya uendeshaji Mbadala wa 1- Ubadilishaji wa Ukuta Mbadala wa 2- Sehemu Wima ya Mbadala wa 3- Sehemu Wima na Nyembamba Wima Matembezi ya Matembezi Athari Bila ya Na Bila ya Na Bila ya Na uboreshwaji uboreshwaji uboreshwaji uboreshwaji uboreshwaji uboreshwaji AWAMU YA ATHARI ZA UENDESHAJI CHINI SANA (+) WASTANI (+) CHINI SANA (+) WASTANI(+) CHINI SANA (+) WASTANI(+) Upatikanaji wa ajira wakati wa shghuli za ujenzi Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Hakika CHINI SANA (+) CHINI (+) CHINI (+) JUU (+) CHINI (+) JUU (+) Fursa za biashara kwa wajasiriamali wa eneo hilo Yawezekana Kiasi Yawezekana Sana Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Hakika Ustawishaji wa usalama wa wendao kwa miguu na CHINI SANA (+) CHINI (+) CHINI (+) WASTANI(+) CHINI (+) WASTANI(+) msongomano Haiwezekani Fairly Fairly Yawezekana Sana Fairly Yawezekana Sana CHINI(+) WASTANI(+) CHINI(+) WASTANI(+) CHINI(+) WASTANI(+) Ukubwa wa msongamano na mzunguko Yawezekana Kiasi Hakika Yawezekana Kiasi Hakika Yawezekana Kiasi Hakika CHINI SANA (+) CHINI (+) CHINI (+) JUU (+) CHINI (+) JUU (+) Ongezeko la majivuno ya kiraia Haiwezekani Yawezekana Kiasi Yawezekana Kiasi Yawezekana Sana Yawezekana Kiasi Yawezekana Sana CHINI SANA(+) CHINI SANA(+) CHINI(+) CHINI(+) CHINI(+) CHINI(+) Rasilimali za kitamaduni na urithi na hali ya WHS Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana CHINI(+) WASTANI(+) CHINI(+) WASTANI(+) CHINI(+) WASTANI(+) Ubora wa Nafasi za Wazi Hakika Yawezekana Kiasi Hakika Yawezekana Kiasi Hakika Yawezekana Kiasi Wasta Wasta CHINI (+) CHINI (+) CHINI (+) CHINI (+) Ongezeko la miti ya minazi Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana CHINI (+) WASTANI (+) CHINI (+) WASTANI(+) CHINI (+) WASTANI(+) Ongezeko la taa za barabarani na samani Hakika Yawezekana Kiasi Hakika Yawezekana Kiasi Hakika Yawezekana Kiasi WASTANI(+) WASTANI(+) WASTANI(+) WASTANI(+) WASTANI(+) WASTANI(+) Utoaji wa huduma Yawezekana Kiasi Yawezekana Kiasi Yawezekana Kiasi Yawezekana Kiasi Yawezekana Kiasi Yawezekana Kiasi CHINI (-) CHINI SANA (-) WASTANI(-) CHINI SANA (-) WASTANI(-) CHINI SANA (-) Uwezekano wa mabadiliko ya kudumu kiuchumi Yawezekana Kiasi Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani Yawezekana Kiasi Haiwezekani CHINI (+) WASTANI (+) CHINI (+) WASTANI(+) CHINI (+) WASTANI(+) Kupoteza au kupunguza matumizi ya katika ufukwe Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana Yawezekana Sana Mabadiliko ya kimo cha ukuta wa kuzuia maji ya bahari CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) (upana na urefu) Hakika Hakika Yawezekana Sana Hakika Yawezekana Sana Hakika Mmomonyoko wa udongo mnyevumnyevu katika vifaa vya WASTANI(-) CHINI (-) WASTANI(-) CHINI (-) WASTANI(-) CHINI (-) ujenzi Very Likely Yawezekana Kiasi Very Likely Yawezekana Kiasi Very Likely Yawezekana Kiasi CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) Makazi ya asili ya ukuta wa kuzuia maji ya bahari Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika Hakika CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) Eneo la baina ya maji kupwa wasta wasta Hakika Hakika Hakika Hakika CHINI SANA (-) CHINI SANA (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) CHINI (-) Mmomonyoko na ufungiaji wa chenga Haiwezekani Haiwezekani Haiwezekani Haiwezekani Haiwezekani Haiwezekani 23 UBORESHAJI: AWAMU YA UENDESHAJI UBORESHAJI: AWAMU YA UJENZI Upatikanaji wa ajira wakati wa uendeshaji 43. Zidisha kuajiriwa kwa watu wa eneo hilo 1. Upatikanaji wa ajira wakati wa shghuli za ujenzi Ongezeko la masoko kwa wajasiriamali wa 2. Kuunda mwongozo wa sera unaoeleweka kwa wafanyikazi eneo hilo wa eneo hilo na kufuatilia ukubalifu wa watoaji huduma 44. Kusaidia wauzaji na maswala ya kupata 3. Tangaza fursa za kazi katika eneo hilo leseni kupitia kwa ZMC 4. Tekeleza shughuli za wafanyikazi bila upendeleo 45. Himiza ZMC kuangalia upya vizuizi kufanya 5. Endeleza ajira kwa mwanamke na wanachama wa jamii ya biashara chini ya mti wa Kibaniani eneo hilo 46. Weka taa za barabarani 6. Rasmisha uandikwaji kazi na kuajiriwa 7. Tekeleza mfumo wa mzunguko Ustawishaji wa wendao kwa miguu na usalama wa msongamano Masoko yaliyongezeka kwa wajasiriamali wa eneo hilo 47. Elimisha waendao kwa miguu kuhusu 8. Saidia katika uwekaji saini katika uanzishaji na uzalishaji Matumizi ya sehemu ya kupita kwa miguu 9. Usizuie ufikivu katika biashara 48. Anzisha elimu ya uvukaji kwa wendao kwa Athari za ongezeko katika uchumi wa eneo hilo na kitaifa miguu 10. Endeleza sera ya uwakala 49. Anzisha mbinu za kupunguza msongamano 11. Unda sajili SMMEs Mzunguko wa msongamano na ukubwa wake 50. Utekelezaji wa mbinu za kupunguza Uwezekano wa uhamishwaji wa kiuchumi kwa muda msongamano katika kila mwisho na katika ya sehemu zilizotambuliwa katika Barabara ya 12. Punguza ukatizaji wa ufikivu katika ufukwe na biashara Mizingani na pia katikati ya vigazi mbalimballi 13. Ruhusu wauzaji kuendelea na shughuli zao za biashara 51. Sanifu barabara yenye upana wa mita 6, ili kupunguza kasi ya msongamano Kumiminika kwa watafutaji kazi 52. Kutekeleza kiwango cha mwendo kasi 14. Sambaza sera ya kuajiriwa vyombo usiozidi mwedo wa 40/saa Upotezaji au upunguzaji wa ufikivu katika ufuo Ongezeko la majivuno ya kiraia 53. Kupachika mabango ya taarifa yanayo 15. Kupunguza ukatizaji wa ufikivu katika ufukwe na biashara onesha kuhusu eneo la mradi pamoja na 16. Kuruhusu umma kuendelea na shughuli zao k.m. uboreshaji wa awali na baada ya uboreshaji Kuogelea 54. Shika doria katika eneo hilo Eneo la Baina ya maji kupwa (Rejelea Sehemu 11.1.2.d) 17. Alama za Nyayo katika upande unaoelekea bahari mwa 55. Pachika na uhifadhi samani za barabarani, ukuta utakuwa na kikomo chake taa za barabarani na visusu vya kutupia taka 18. Vizuizi na majengo ya kasha yanafaa kuchukuliwa ili kuonyesha mwisho wa eneo la ujenzi na hakuna Rasilimali za kitamaduni na Urithi na Hali ya mfanyikazi anafaa kushughulikia katika upande huo Sehemu ya WHS unaoelekea baharini 56. Linganisha vifaa vya ujenzi wa ukuta wa 19. Uchimbaji unafaa kudhibitiwa hadi katika ukubwa kuzuia maji ya bahari pamoja na mwonekano unaohitajika wake mwisho na ule uliotumika katika Bustani ya Forodhani Yenye Kuvurugika - Hakuna 57. Endapo ubadilishaji ardhi utatekelezwa nafasi Kelele na uchafuzi wa hewa (vumbi) ya ukuta uliopo inafaa kutambulika kwenye 20. Kupunguza saa za ujenzi usanifu na kwa kutumia ya uwekaji wa alama 21. Harakisha kule kuhamishwa upya kwa IPA iliyo tafsiriwa 22. Lazimisha na fuatilia sheria zinazohusiana na kelele inayosababishwa na wafanyikazi wa ujenzi 58. Hatuwa zichukuliwe kutafsiri na kuunganisha nafasi kutoka kwenye ukingo wa bahari hadi Mitetemeko kwenye sehemu ya Mji Mkongwe. 23. Usanifu wa mwisho kuelezea mbinu za ujenzi na kiwango Ubora wa Nafasi Wazi kinachokubalika cha mitetemeko 59. Hakikisha mandhari mwafaka na uhifadhi wa 24. Kutekeleza uchunguzi kamilifu wa ujenzi ili kuelewa hali maeneo ya mandhari zinazoambatana na matayarisho ya ujenzi 25. Fuatilia mitetemo na athari katika majengo yaliyopo kando Kuongezea miti ya mnazi Hali ya kuwa Mahali Hakuna hatua za uboreshaji ambazo zimetambuliwa, hata hivyo uangalifu unafaa 26. Kutumia mipaka wa eneo la matangazo ili kuwasiliana kuzingatiwa katika uchaguzi aina za miti ya kuhusu mradi, kuupamba kwa sanamu nzuri za mnazi ili kuhakikisha upenyezi wa mwangaza. kufurahisha za eneo au picha za mandhari ya mbele ya bahari Athari katika kuongezea taa za barabarani na samani Rasilimila za Urithi 60. Uchaguzi wa vifaa vya taa na samani unafaa kuwa katika kuendeleza majengo 27. Hakikisha yasiyo ruhusiwa kupita yametengwa wazi na yanayozunguka eneo hilo na Bustani ya kuwekewa alama zinazo zuia kufika Forodhani 28. Daftari la maoni na manunguniko ya umma inafaa kuwekwa katika eneo wakati wa awamu ya ujenzi 61. Mwangaza unafaa kuelekezwa chini na 29. Mamlaka ya Uhifadhi na Maendeleo ya Mji Mkongwe kando ya barabara na wala si juu na nje yanafaa kufikishiwa mawasiliano mara moja endapo kuelekea kwenye bahari kutagunduliwa uharibifu wowote kutokana na shughuli 24 hizo. Utoaji huduma Hakuna hatua za uboreshaji ambazo zimetambuliwa, ingawaje inafaa kukumbukwa kwamba athari chanya zinazohusiana na huduma ya miundo mbinu hazitegemei Mti wa Mabaniani utekelezaji wa siku za usoni na muunganisho huo 30. Punguza uharibifu wa mfumo wa mzizi kwa kuzuia uchimbaji ambao ni wa kupindukia Ufikivu katika ufukwe 31. Pindi mizizi mikuu itakapogunduliwa usaidizi kutoka kwa 61.Pointi za kufikia ufukwe kulingana na usanifu wataalam wa mizizi waliofuzu unafaa kutafutwa kuhusiana zinafaa kuwezesha ufikivu katika ufukwe wa watu na mbinu bora na mwafaka za kukabiliana nazo. na hata mashua Utembeaji wa mwenda kwa miguu 32. Kutenga eneo wazi na vizuizi, vyote vinafaa kupachikwa ili Uwezekano wa uhamishwaji wa kudumu kuwezesha utembeaji mzuri wa waendao kwa miguu wa kiuchumi 33. Utembeaji kando ya ufukwe unafaa kuwa salama na uliodhibitiwa 62. Hakuna vizuizi vya ziada vitakavyowekwa katika eneo la mradi Mzunguko wa msongamano 63. Tilia maanani mapendekezo ya jamii maelezo 34. Liwekwe bango linalosomeka kwa urahisi likionyesha hali ya usanifu katika mradi halisi ya barabara na njia mbadala 64. Usanifu wa mwisho unafaa kuwa na 35. Mbinu mwafaka za usimamizi wa msongamano ama uwezekano mchache zaidi wa athari katika mwisho wa eneo la ujenzi zinafaa kuwekwa kwa pale pa ufukwe kugeuza magari 36. "Mfumo wa simama-na-nenda" uwekwe ili kuwezesha Kubadilishwa kwa ukubwa wa ukuta wa ufikivu na utokaji wa magari ya ujenzi kuzuia maji ya bahari (urefu na upana) 37. Hakuna ujenzi mwengine utaoruhusiwa wakati huohuo katika Barabara ya Mizingani Hakuna hatua za uboreshaji 38. Utekelezaji wa kina wa njia moja kwa ufikivu wa Barabara zilizopendekezwa kama usanifu wa "vitofali ya Mizingani; vya juu" havina urefu, vimeoanishwa na hali ya umbile, rangi na tayari imekatwakatwa Vizuizi kuhusiana na maegesho katika mwonekano wake. upana wa njia ya waendao kwa miguu ni kulingana na na 39. Kutoa vocha za maegesho/vibali kwa wenye ardhi, nafasi iliyopo kwani ukuta wenyewe wapangaji na watumiaji waliopo wa kila siku katika kipindi haujasogezwa, hakuna hatua za uboreshaji kile cha ujenzi zimetambuliwa. 40. Jadili kuhusiana na maegesho ya bure kwenye eneo la Kibaniani wakati wa jioni Mmomonyoko wa kinyevunyevu katika majengo Ukatizaji wa Huduma 65. Matumizi ya sehemu ya kupitisha au ya kupitisha nusu maji katika sehemu ya 41. Utekelezaji wa mpango wa usimamizi wa kimazingira na kutembelea kando ya majengo yoyote kijamii kushughulikia taratibu za usimamizi kwa ajili ya usumbufu wa huduma na usimamizi wa usafishaji wa 66. Pembe ya sehemu ya kutembelea ili kwamba dharura. mtawanyo-nyuma uwe na mipaka na 42. Urajisi wa manunguniko ya umma kwamba maji yanatiririka kutoka na si kando au kuelekea kwenye majengo 67. Kufuatilia afya ya ukuta wa mbele huku lengo mahsusi likiwekwa kwenye mmomonyoko wa udongo mnyevumnyevu Makazi ya asili ya ukuta wa kuzuia maji ya bahari Hakuna hatua za uboreshaji zimetambuliwa Eneo Baina ya maji kupwa 68. Safisha ulinzi katika msingi wa ukuta ili uwe na tambara tumbawe Ugongwaji na mmomonyoko wa chenga Hakuna hatua za uboreshaji zimetambuliwa 25 Hatua za uboreshaji zilizofafanuliwa hapo juu zimewekwa ndani kwa ndani katika Mpango wa Usimamizi wa Kimazingira na Jamii (ESMP) katika mradi (rejelea kiambatisho L) na ambapo husika, katika mazingira ya mkataba ulotolewa kwa Makandarasi. Hatua lazima ziwekwe sawa ili kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa hatua hizi na kuchukua hatua sahihishi pale panapohitajika. 1.5 MUHTASARI WA UTATHMINI Jumla ya athari zenye uwezo 17 katika awamu ya ujenzi na nyingine 17 katika awamu ya uendeshaji zilitambuliwa (rejelea Jedwali la 3 hapo juu). Katika kuchambua umuhimu wa vipimo kabla na baada ya uboreshaji yafuatayo yanaonekana wazi: Awamu ya Ujenzi · Inazo athari hasi zaidi kuliko chanya wakati wa ujenzi (chanya tatu na hasi kumi na nne) · Hatua za uboreshaji za kutosha zinatarajiwa katika wakati wa ujenzi ili kuonekana wazi kwa athari chanya hadi katika viwango vinavyokubalika huku athari chanya kwa wastani zikiendelezwa ili kufikia faida za juu zaidi katika jamii zinazozungukia eneo hilo; na · Athari za ujenzi za Mbadala wa 2 kwa kiasi fulani zinazo faida kubwa zaidi kuliko Mbadala 3 ambao ni bora zaidi kwa kiasi fulani kuliko mbadala 1. Awamu ya uendeshaji · Inazo athari nyingi za maendeleo zaidi za chanya kuliko hasi kwenye awamu ya utendaji (chanya kumi, hasi saba) · Kwamba hatua za uboreshaji za kutosha zinatarajiwa ili kupunguza umuhimu wa athari asili hadi katika viwango vya kukubalika, huku athari chanya kwa wastani zitaweza kuendelezwa pakubwa ili kuongezea kwa kiasi kikubwa faida katika jamii zinazozungukia eneo hilo; na · Athari za uendeshaji za Mbadala wa 2 zinazo faida zaidi kwa kiasi fulani kuliko Mbadala wa 3 ambao ni bora zaidi kwa kiasi fulani kuliko mbadala wa 1 Matokeo ya uchaguzi mdogo wa athari kimazingira kwa kuzingatia matokeo ya ESIA hivyo basi ni Mbadala wa 2 yani ukuta wima na sehemu ya matembezi. 1.6 MAPENDEKEZO Hatua za uboreshaji maalum zilizotolewa katika sehemu 12.1 pamoja na maelezo yaliyomo katika ESMP yanaitikia maswala yaliyozungumziwa kuhusiana moja kwa moja na mradi pendekezwa. Yanalenga katika kupunguza athari, kutilia mkazo faida 26 na kuepuka uharibifu usiofaa wala kustahili katika mazingira ya kawaida ya kitamadini na ya kiuchumi-jamii. Inapendekezwa vikali kwamba hatua hizi zijumuishwe katika mahitaji ya uhamishaji, utekelezaji na ufuatiliaji. Kulikuwa na mitazamo ya ziada kadhaa, hata hivyo, ambayo ilizungumziwa wakati wa ESIA ambayo ni mapendekezo ya kuangaliwa zaidi na STCDA pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari ili kuhimiza hali hizi katika mradi katika kuonekana kwa mradi au kuepuka uharibifu usiokusudiwa. Yameorodheshwa hapa chini. Taka · Yamkini, jamii zinazozungukia eneo hilo mara kwa mara hutupa taka zao za nyumbani kwenye bahari katika eneo hilo la mradi. Hali hii hufanywa mara nyingi wakati ambapo manispaa haikusanyi taka katika nyumba za watu. Aidha ufukwe kwa sasa hivi unasafishwa mara moja kwa wiki na mtu binafsi wa eneo hili kwa ada maalum inayokusanywa na wasimamizi wa mashua na wavuvi kutoka katika biashara mbalimbali na watu binafsi walio karibu na eneo hilo la mradi. Ukusanyaji wa mara kwa mara wa taka na uwajibikaji mahususi wa kuondoa takataka kutoka katika ufukwe utafanya mahali hapa pawe penye afya zaidi na pa kupendeza. Taka ambazo hazijakusanywa nje ya mkahawa wa Mercury 27 Faida za ziada za jamii · Wendeshaji mashua na wavuvi walionyesha kwamba mbali na hatua za uboreshaji za moja kwa moja zinazohusiana na mradi zipo pia faida za ziada ambazo zinaweza kutolewa na zinajumuisha: o kwa kupewa vifaa vya uvuvi na ya ziara za kitalii pamoja na kisanduku cha huduma ya kwanza o kwa kuwa na mahali mahususi au chombo fulani ambacho wataweza kutia nanga na kufunga mashua yao. o Kwa kuwekwa vyoo vya umma mahali fulani katika eneo maalumu la kufanyiwa utafiti o Kwa kuwa na mpango wa kuelimisha jamii maswala ya kimazingira ambapo wazazi pamoja na wanafunzi watafunzwa kuhusu maswala ya kimazingira pamoja na athari ya kutisha inayotokana na kutupa taka katika bahari. Eneo Duara la Mti wa Kibaniani · Ilitiliwa maanani kwamba mti wa Mabaniani haupunguzwi matawi katu na inaaminika na wenyeji kwamba hali hii inasababisha haswa kuongezeka kwa idadi ya mbu. Usimamizi unaofaa katika mti huo wa Baniani unafaa kutekelezwa · Uboreshwaji wa mzunguko wa msongomano unafaa kutiliwa maanani pia haswa mipangilio ya karibu na eneo duara la mti wa Kibaniani. Labda kwa hali ya mduara wa msongamano ili kuwezesha magari kugeukia hapo. · Iligunduliwa kwamba wakati wa utafiti wa kuboresha ukuta wa kuzuia maji ya bahari, kulikuwa na athari kuu katika msongamano wa eneo hilo kutokana na shughuli za bandari. Shughuli hizi ziliendelezwa hadi katika eneo duara la Mti wa Kibaniani na hata mpaka eneo la sehemu ya mbele ya bahari. Kama ilivyoelezwa awali, sehemu ya mbele ya bahari ilionekana kuwa pahali pa maegesho haswa ya malori yanayosubiri, hali isiyopendeza haswa katika eneo ambalo ni la urithi na kitalii. Inapendekezwa sana kwamba shughuli za msongamano katika Bandari na kati ya Bandari hadi katika eneo la Eneo Duara la Mti wa Kibaniani zinafaa kufanyiwa utafiti kwa mtazamo wa kuunda mazingira bora zaidi yenye uendelevu. 28 Eneo Duara la Baniani (kushoto) na kiingilio cha bandari baada ya kuwasili kwa meli (kulia) Kuimarisha mambo Urithi · Miongozo ya maelezo ya usanifu wa majengo kando ya Barabara ya Mizingani unafaa kutayarishwa ili kusimamia uhifadhi wa hali halisi ya ufundi sanifu wa Barabara. · Hatua za kufasiri na kuunganisha nafasi kutoka pembezoni pa bahari hadi katika Mji Mkongwe zinafaa kutiliwa maanani. 1.7 MBADALA PENDELEWA Hitimisho inayotolewa kutoka katika meza ya tathmini na muhtasari wa majedwali yaliyotathminiwa umuhimu wa vipimo vya wazi inaonyesha kwamba mibadala yoyote ile itakayoteuliwa, athari zinaweza kuboreshwa na kwamba faida za kijamii kwa kiasi kikubwa zinazidi ule uwezekano wa hasara zitakazokuwepo. Aidha muhtasari mwingine uliofikiwa na kuafikiwa ni kuhusu hali ya sehemu ya waendao kwa muguu kutoa fursa zaidi kwa kuleta faida kuliko mbadala ambao unabadilisha tu ukuta wa kuzuia maji ya bahari uliopo hivi sasa. Athari za kiekolojia zilipatikana kuwa karibu sawa sana na machaguo ya sehemu ya waendao kwa miguu mbali na yanaonekana kuwa na umuhimu wa chini kwa jumla. Faida za kijamii zinategemea uendelezaji wa kisanifu ambao unalenga usalama wa wendaao kwa miguu na unahakikisha ufikivu bora zaidi na unaoendelea hivyo katika ufukwe. Faida za muda mrefu au kipindi kisichokuwa kifupi kwa watumiaji wa hivi sasa na jamii inayozungukia eneo hilo, zitatiliwa nguvu kama uendeshaji na usanifu haukatizwi shughuli za mtumiaji wa hivi sasa na ufikivu wake katika eneo lakini zinalenga katika kuboresha ubora wa nafasi wazi ambayo imependekezwa. Mbadala uliopendelewa ni Mbadala wa 2 ambao unaelezea kuhusu ukuta wima wa kuzuia maji ya bahari ulio na sehemu ya matembezi kwa maana inatimiza malengo 29 ya kisheria ya kisera, kimazingira, kimpangilio na uhifadhi tukichukulia ya kwamba hizo hatua za uboreshaji na mapendekezo yaliyotolewa vyote vitaweza kutekelezwa na kufuatiliwa ifaavyo. Kwa kurejelea taarifa iliyopo katika awamu hii ya mzunguko ya mpango wa mradi (yaani usanifu wa maelezo ya awali), ujasiri katika utathmini wa kimazingira uliotolewa unatazamwa kama njia inayokubalika katika kutoa uamuzi, hususan kulingana na athari na hatari za kimazingira. Hata hivyo, inatambulika kwamba maelezo ya maendeleo yaliyopendekezwa yataweza kukua kwenye kipindi kile cha wakati wa awamu za ujenzi na usanifu. Hata hivyo, huenda hali hii haitabadili ukubalifu wa jumla wa kimazingira wa mradi huu uliopendekezwa. Kupotoka kokote kwa kiasi fulani kutoka katika kile kilichotathminiwa katika EIR hii kunafaa kutegemea utathmini wa zaidi na huenda ukahitaji mabadiliko katika Uidhinishaji wa Kimazingira, baada ya mchakato uliopangiliwa kutimizwa na kumalizwa vizuri. Mbadala uliopendelewa ni Mbadala wa 2 ambao unaelezea kuhusu ukuta wima wa kuzuia maji ya bahari ulio na sehemu ya waendao kwa miguu kwani unaweza kutimiza malengo ya kisheria, kisera, kimazingira, kimpango na ya uhifadhi tukichukulia kwamba hatua hizo za uboreshaji na mapendekezo yaliyotolewa yatatekelezwa na kufuatiliwa ifaavyo. Kulingana na mabadiliko yaliyowasilishwa kuhusiana na vidaraja na upana wa kijia katika upande wa jengo la barabara inakubalika kwamba njia ya waendao kwa miguu ni pana zaidi dhidi ya ile ya majengo itafaidi ule uhifadhi wa kuta za mbele ya jengo. Inaeleweka zaidi kwamba kufanya barabara kuwa nyembamba kutasababisha magari kupunguza kasi yao kiufundi bila kujua. Ukichukulia kwamba magari ambayo si ya magurudumu yataweza kufikia hiyo sehemu ya matembezi nafasi finyu ya barabara kwa vyovyote vile haihatarishi usalama wa watumiaji hawa. Vilevile upana ule ulioongezeka wa ujia ule katika upande wa jengo unaweza tu kufaidi kuta za mbele zilizopo kando. Kutokana na hayo Mbadala wa 3 wa Sanifu ambao ndio chaguo pendelewa la shabiki unaoenekana kukubalika kimazingira. Kwa mujibu wa mabadiliko ya vigazi vya Mercury sehemu muhimu zaidi ni ile ya wepesi wa kufikia hadi mwisho na kuongezeka kwa chelezo cha mashua ambayo ni maarufu katika mitawanyo yote mitatu. Na kwa hivyo mibadala yoyote ile mitatu ya vigazi inaonekana kukubalika pamoja na mbadala wa tatu uano pendelewa, na inaweza kuteuliwa kutegemea na kanuni za mpango na za urembo ama uzuri wa eneo lote. Hivyo basi ni maoni yetu kwamba, tukiwa Wataalamu Huru wa Utathmini wa Kimazingira, uboreshwaji na ukarabati uliopendekezwa wa Mbele ya bahari ya Mizingani uidhinishwe. 30